Tafuta katika Blogu Hii

Jumatatu, 6 Aprili 2015

HIVI NDIVYO MAJI YENYE TAKA YANAVYOPITIA MFUMO WA USAFISHWAJI KABLA HAYAJATUMIKA



Hapa nitazungumzia maji tunayotumia kila siku kwa matumizi ya nyumbani .
Nchini Tanzania maji tunayotumia hutokana na vyanzo mbali mbali vya maji hasa mito na maziwa , pia kuna mabwawa ya kutengenezwa  mfano bwawa la mindu ambapo pia bwawa hilo hutegemea sana maji kutoka kwenye mito mbali mbali inayotililisha maji kutoka milima ya uruguru . Wizara ya maji ndio imepewa jukumu kubwa hasa la kusimamia na kuendeleza vyanzo hivi kwa umuhimu w taifa letu kiujumla .
Hivyo wizara imegawanya vyanzo hivyo vya maji katika mabonde lakini mada hii haitazungumzia juu ya hayo mabonde .
Maji kutoka kwenye chanzo hubeba vitu mbali mbali ambavyo ndio taka  kama vile mizoga ya wanyama , miti iliyo angushwa na mvua au kwa nji yeyote , vinyesi vya wanyama akiwemo mwanadamu , uchafu kutokana na shughuli mbalimbali za watu kama nyavu za uvuvi , nguo nguo ,  na hata vijidudu viletavyo magonjwa na ata utupwaji wa taka za viwandani .  

ZIFUATAZO NI HATUA ZINAZOFANYIKA ILI KUWEZA KUPATA MAJI YALIYO SAFI NA SALAMA

HATUA ZA AWALI


1 Maji hupita kwenye machujio makubwa au ya kwanza ambapo ukilejea kwenye utangulizi utagundua kuwa maji hubeba taka zenye ukubwa tofauti tofauti hivyo kazi kubwa hasa ya hayo machujio ya kwanza ,
Hivyo baadhi ya taka ndogo ndogo zinaweza kupenya .
Basi watalamu wa maji baada ya kuona hilo wakatengeneza machujio mengine ambapo zile takandogo ndogo zilizo pata nafasi ya kupenya kwenye machujio ya kwanza hapa zimezuiliwa hivyo hubakia chembechembe za taka ambazo  si rahisi kuzichuja kwa hivyo hatua ifuatayo itaonyesha jinsi ya kuondoa hizo chembe chembe za taka



2.Kitaalamu inaeleweka kwamba chembe chembe ndogo za uchafu hubeba chagi hasi hivyo ili tuweze kuziondoa tunahitaji chagi chanya ambapo kitaalamu huitwa coagulant
Kwa hiyo coagulant ni kemikali inayowekwa kwenye maji ili kuungana na chembe ndogo ndogo za uchafu zenye chagi hasi , mfano wa hizo chemikali ni kama Alum au alminuam sulfeti pia ipo nyingine huitwa algae floc ,

3. Hatua hii husisha tanki ambalo linaluhusu maji yetu pamoja na coagulant vipate kuchanganyika na kitendo hicho usababisha chagi hasi na chanya ziungane na kutengeneza mabonge mabonge ya muungano hali hiyo huleta uzito hivyo madonge hayo hushuka chini kabisa ya tanki(basin) ambapo kitaalamu tunasema settlement .
Maji yetu hujitenga mbali na hayo madonge na kuonekana yenye utulivu  kwa juu

HATUA ZA UPILI
 4.Tunanahitaji maji yaweze kujitenga mbali na madonge yaliyo jitenga chini kabisa ya tanki hivyo hatua hii huitwa hatua ya mchujo (filtration) ambapo mji yetu hupelekwa kwenye tanki lingine ambapo kuna vichujio vinavyo husisha leya ya mchanga na leya ya grevos ambapo chembe ndogo za uchafu huchujwa  na madonge ambayo hutolewa na kupelekwa pembeni au dampo maalumu

5. Baada ya hapo maji yetu huonekana yako safi kwa ajili ya kutumia lakini hayapo salama kwa afya zetu kwa sababu bado yatakuwa na vimelea vya magonjwa, kama vile bacteria , virusi amiba nakadhalika , hivyo tunahitaji kuviondoa au kuviua ,hapa ndipo tunahitaji dawa ya kuyatibu maji yetu na kitendo hiki kitaalamu huitwa( disinfection)
Dawa inayoonekana kufanya vizuri zaidi hapa huitwa klorini ambayo inaweza kuwa katika mfumo wa gesi au kimiminika , ingawa mionzi inaweza kutumika kama vile ,
Ultravioleti na Ozoni ,lakini sababu kubwa inayofanya hii kemikali ya klorini iwe bora kuliko zingine ni kwamba inauwezo wa kubaki ikisafiri pindi maji yetu yanapoelekea kwenye jamii ya watumiaji , kwa sababu mipira ya kusambazia maji kuna wakati hupasuka maji yakiwa njiani hivyo  vijidudu hasa bacteria hupata nafasi nyingine ya kudhuru maji yetu hivyo kiasi kidogo sana na kilichopimwa kilicho kati ya mililita 0.2 hadi 0.5 cha dawa hushugulikia hivyo vijidudu .

6. Baada ya hapo maji yetu hupelekwa kwenye tanki kubwa sana ambalo huweza kumudu kubeba maji zaidi ya milioni elfu moja za lita kwa siku kwa ajili ya matumizi ya jamii husika
Hapo ndio mwisho wa jinsi ya kupata maji safi na salama kwa ajiri ya matumizi yetu ya kila siku , ingawa mfumo huu hugharimu kiasi kikubwa sana cha pesa katika kutengenezwa na kufanya ripea hivyo ni muhimu kufanya uangalizi wa mara kwa mara
 Uangalizi huusisha kusafisha machujio baada ya uchujaji kumalizika , kitendo hicho kitaalamu huitwa ( backwashing) tunahitaji kusafisha ili yasije yakaziba na kusababisha hasara na ufanisi usiotakiwa wa mtambo .

Pia uangalizi mwingine ni juu ya kiwango cha dawa ya klorini ambayo inatakiwa ibaki kwenye maji , harufu ya maji , na hata asidiki na ukakasi wa maji



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni