Tafuta katika Blogu Hii

Jumapili, 6 Septemba 2015

KUENEA KWA UGONJWA WA KIPINDUPINDU NA MATUMIZI YA MAJI


Hivi karibuni kumeibuka kwa ugonjwa wa kipindupindu katika jiji la Dar es salaam hasa wilaya ya kinondoni ikishika nafasi ya kwanza kwa kuwa na wagonjwa wengi , ugonjwa huu husababishwa na bacteria anayeitwa vibrio  cholerae , bacteria huyu hupatikana kwenye kinyesi cha binadamu , hivyo ili upate ugonjwa huu ni lazima utakuwa umekula kinyesi pasipo kujua pia ugonjwa huu huenezwa na mawakala wa uchafu hapa nazungumzia mdudu anayeitwa nzi ambaye hupenda kusogelea maeneo machafu hasa yenye vinyesi vya wanyama , huwenda ulikula tunda ambalo halikuoshwa ipasavyo au chakula ambacho hakikuhifadhiwa vizuri hivyo nzi mawakala wakatua kwenye chakula na kuacha vimelea vya magonjwa , lakini kikubwa zaidi matumizi ya maji ambayo si salama kwa kunywa , niliwai kutembelea baadhi ya maeneo ya jiji nikiangalia au kukagua ni kipi kisababishi cha ugonjwa huu wa kipindupindu yapo mengi niliyojifunza lakini kikubwa hasa ni swala zima la mazingira machafu katika maeneo ya nayozunguka nyumba za watu au sehemu za kibiashara kama sokoni




 

SABABU ZIFUATAZO ZILINIFANYA KUANDAA MADA HII KAMA KISABABISHI

 

1.Miundombinu mibovu ya mfumo wa maji taka na maji safi

Jambo hili nimewahi kuliongelea sana , miundombinu chakavu ya maji taka usababisha maji taka kukutana na yale yaliyokuwa safi , uwenda ni yale yaliyotibiwa na dawasco au visima vifupi ambapo watu wamekuwa wakitumia maji hayo ya visima vifupi wakijua ni chemichemi kumbe ni kuvilia ndani kwa ndani kwa maji taka lakini hili linaenda sambamba na ukosefu wa vyoo bora katika baadhi ya maeneo , kuna maeneo ukiingia chooni unaweza ukagairi kujisaidia hata kama ungebanwa vipi na haja , vyoo chakavu vilivyofikia hatua ya kutapika ni rafiki kwa nzi wa kijani kubeba vimelea vya magonjwa hasa kipindupindu  

 
 

2. uwepe wa maji taka karibu na makazi ya watu

Kuna maeneo mengi sana katikati ya jiji la Dar es salaam ambapo ni kawaida kukuta maji machafu yakituama kandokando ya makazi ya watu huku kukiwa na shughuli mbalimbali zikiendelea kama huduma ya vyakura maarufu kama mama ntilie ,hii pia ni hatari kwa watoto wadogo ambao wakati mwingine huona maji hayo kama ni sehemu tu ya michezo yao , huenda wasifikie hatua ya kuyatia kinywani lakini uwezekano wa kugusana nayo mikononi ni mkubwa hivyo wazazi nao wasipokuwa makini mtoto anaweza kula kitu kingine bila ya kunawa mikono na kusababisha kupata ugonjwa , sababu hii inaweza kuwa ya msingi kwa sababu takwimu zimeonyesha kuwa miongoni mwa wagonjwa watoto wamekuwa wengi ukilinganisha na idadi ya watu wazima

 

3 .watu kutozingatia kanuni za afya asa usafi binafsi , mfano kula chakula bila kunawa vizuri , kunywa maji yasiyotibiwa au kuchemshwa , pia kama nilivyosema kuhusu watoto ambao awapatiwi uangalizi wa kutosha kutoka kwa wazazi wanapokuwa katika michezo au katika maswala mazima ya ulaji

 

4. mkusanyiko mkubwa wa watu katika eneo moja ,

Hapa ndipo chanzo cha ugonjwa , kukua kwa kasi kwani utagundua nyumba moja ya kupangisha inaweza kuwa na watu wengi au kukaribiana bila nafasi kati ya nyumba na nyumba hivyo unaweza kuona maeneo hayo maarufu kama uswailini , wakati mwingine uwezi kutofautisha kuwa choo Fulani ni cha nyumba hipi , mifumo ya maji taka mara zingine huingiliana kati ya nyumba na nyumba  kiasi kwamba tabia za baadhi ya watu kutozingatia kanuni za afya upelekea kupatwa na ugonjwa , lakini kwa sababu watu wamekusanyika eneo moja ni rahisi sana kwao kuambukizana , hivyo ni vizuri watu wakajaribu kuishi katka maeneo yenyempangilio wa makazi bora unaoleta maana ya kuishi , mfano mzuri ni wilaya ya ilala ambapo si mara chache sana hupatwa na kipindupindu ,ingawa pia yapo maeneo hatarishi lakini maeneo mengi yamepangilika kimakazi  

 

NINI KIFANYIKE KATIKA KUKABILIANA NA UGONJWA HUU HATARI

Katika kutatua au kupambana na tatizo hili kiuna makundi ya kijamii mashirika binafsi na serikali

1 kijamii

   Swala la usafi wa mazingira linaanza na mtu mmoja mmoja , hasa katika ngazi ya kifamilia , tuache kuwa wavivu wa kukemea au kusemana kuhusu usafi katika maeneo yetu tunayoishi , pia tuache dhana ya kuilaumu serikali bila kufanya sehemu yetu, kama mwanajamii tunawajibu wa kulinda miundombinu ya maji , wapo watu hukata kwa makusudi mipira ya kusambazia maji safi ili ajinufaishe wao , si gharama pekee itakayoingia serikali kufanya matengenezo bali itapelekea kuingiliana kwa mifumo ya maji safi nay ale ya maji taka

 

2 serikali au sekta zisizo rasimi nazo zinaweza kuchangia kuenea kwa ugonjwa kwa namna moja au nyingine , mfano yapo maeneo ambapo hakuna ufatiliaji juu ya miundombinu chakavu inayopitisha maji safi na maji taka ili kujua wapi kuna mipasuko inayo sababisha maji yawe na vimelea vya ugonjwa , hivyo sampuli za maji zichunguzwe kila baada ya mda Fulani kujua kama kuna uchafuzi wa maji au la

Pia mamlaka husika kama wizara ya afya inajukumu kubwa la kuhakikisha elimu ya kutosha inawafikia watu ili wawe na mitazamo mizuri kuelekea afya na mazingira yao.