Tafuta katika Blogu Hii

Jumapili, 12 Machi 2017

FAHAMU KUHUSU MAJI NA SAYANSI YAKE.BLOG SPOT.COM


Lengo la blogi hii  ni kusaidia na kutoa elimu kwa jamii , hii ni blogi bora ya sayansi Tanzania na Afrika mashariki imeanziswa tarehe 21 /03/2015 ikianza na wasomaji zaidi ya hamsini kwa siku huku ikikua kwa kasi


Blogi hii imejikita katika utafiti na kutatua changamoto  zinazokumba jamii  katika maeneo mbalimbali  ya nchi haswa swala zima la  upatikanaji wa maji safi na salama  ,kutoa ushauri wa kiteknologia kwa watu wenye kampuni vikundi na hata mtu mmoja mmoja wanaojihusisha na biashara ambazo hukutana na changamoto katika swala zima la ubora wa maji au matumizi ya maji kiujumla mara nyingi swala zima la ubora wa maji limekuwa likimulikwa kwa tochi au kutopewa kipaumbele hasa nchi zetu zinazoendelea na watu wengi wanapoona maji yanapatikana kutoka kwenye vyanzo vyao huzania wamemaliza changamoto ,

 lakini ukweli unabaki kuwa maji yanaviambatanishi vingi vinavyoweza kuleta madhara katika afya zetu katika biashara zetu ,viwanda vyetu na ata  katika ujenzi mfano maji yabisi yanaweza kuleta madhara makubwa kwenye mitambo ya kupozea au ya kuchemshia ( boilers), kulika kwa chuma . au chumvichumvi kuganda kwenye kuta za chuma na hivyo kupunguza ufanisi wa mitambo hiyo hii hughalimu makampuni makubwa kiasi kikubwa cha fedha kutatua tatizo au hulazimika kuagiza mitambo mingine  mfano wa mitambo hiyo ni ile inayo tumika kwa ajil ya kufua umeme

 Pia kiafya maji yenye madini tembo yanaweza kusababisha kansa kwa mtumiaji kama yataonekana kwa kiwango kidogo tu pia maji yanaweza kuwa na wadudu hatarishi kiafya , ukuaji wa viwanda na maendeleo ya kiuchumi huchangia kwa kiasi kikubwa katika uchafuzi pale ambapo madini sumu yanapotumika kwenye utengenezaji wa vifaa kama kompyuta , vifaa hivi vinapochakaa , uteketezaji wake unaweza usiwe katika kiwango ambacho ikazuia yasikutane na vyanzo vya maji

Pia tunatoa ushauri juu ya kusafisha na kutibu maji ikitegeme dhumuni lako katika matumizi ya maji hayo

Mfano

Maji kwa matumizi ya kunywa
Maji kwa matumizi ya umwagiliaji
Maji kwa matumizi ya kujengea
Maji kwa matumizi ya viwandani
Maji kwa matumizi ya ufugaji

Pia  wasiliana nasi kwa mahitaji mbali mbali vinavyohusu uchimbaji visima nakadharika