Tafuta katika Blogu Hii

Jumapili, 20 Machi 2016

MAJI BORA KWA AJIRI YA UMWAGILIAJI



Maji ni muhimu sana kwa ajili ya umwagiliaji , katika dunia hii hasa nchi zinazoendelea, ufanisi na ubora katika swala zima la kilimo ni jambo linalotazamwa kwa karibu sana , tumefikia wakati ambapo hatuwezi tena kutegemea mvua ili kufikia kwenye dhima ya uzalishaji bora , hatuwezi tena kutumia jembe la mkono , pia ardhi yenye rutuba ni jambo la kutazamwa kwa karibu sana , watu wengi hukumbuka mambo mengi ya msingi wanapofikilia kuanzisha mradi wa kilimo cha umwagiliaji lakini hawaweki mkazo hasa katika swala zima la ubora wa maji, wengi wetu huamini tu kuwa kama maji yanapatikana eneo husika basi inatosha yatumike katika mradi , jambo hilo si sahii kwa sababu maji yanaviwakilishi vingi ambavyo havihitajiki katika mmea ili uweze kukua , hivyo lengo la blogi hii ni kukupa ushauri wewe mkulima uliye na ndoto za kuvuna mazao yaliyo bora pale utakapo fahamu juu ya ubora wa maji yako , kwani maji yanaweza kuwa na viwakilishi vyenye sumu kali kama vile madini tembo ,unaweza kuwasiliana nami kupitia barua pepe yangu ambayo ni mackthekwembe@gmail.com kwa maelezo zidi .