Tafuta katika Blogu Hii

Jumapili, 17 Mei 2015

JINSI YA KUJUA MAJI NI SAFI NA SALAMA KWA MATUMIZI





Unapotaka kujua kuwa maji yako yanafaa au hayafai kwa matumizi lazime kuzingatia kuwa ni nini kusudi la kutumia maji yako .Je ni kwa ajiri ya kunywa na matumizi ya nyumbani , kwa ajiri ya ujenzi , au kwa ajiri ya mapuli ya kuogela ?


Maji kabla hayajatua katika gamba la juu la dunia yakiwa kama mvua yanakuwa katika usalama ila pale yanapoifikia tu ardhi ndipo uhakika wa usalama wake ni sifuri , hii ni kwa sababu kuna mgusano wa mambo mengi ambayo yapo ardhini na maji yanapoifikia ardhi , mfano kuna madini mbali mbali kama vile aluminiam ,calcium na chembechembe za kioganiki , bila kusahau bacteria mbalimbali , ambao ukaa kwenye vinyesi vya wanyama damu moto mfano vibrio cholera . lakini ni mara ngapi tumewahi kuhisi au kuamini kuwa maji ya chanzo Fulani kama chemichemi ni safi na salama na wakati mwingine tumejalibu kunywa bila hata kuchemsha ?  hasa sehemu za vijijini watu wengi wamekuwa wakiishi kwa mazoea , hii imefanya ata kinga zao kukubaliana na mazingira ya maji wanayo yatumia , bila kuhisi kuumwa kwa muda mrefu , lakini angalizo ni kwamba , watu hao wapo kwenye hatari ya kuugua magonjwa yanayotokana na maji kama vile kipindupindu



Je tutajuaje sasa kuwa maji tunayoyatumia ni safi na salama ?

Hapa nitaelezea hatua za awali mbaka ile ya mwisho ambayo itatupatia hitimisho 



1 KUFAHAMU CHANZO CHA MAJI HUSIKA


Chanzo gani ambacho kina maji yanayotumiwa , chanzo kinaweza kuwa mto , ziwa au bwawa la kutengenezwa , kisima ,bomba la maji yakusambazwa au maji ya bahari , lengo la kujua chanzo kinaweza kutupa historia ya eneo husika , lakini kikuubwa zaidi ni ili tupate kuchukua sampuli ambayo itawakilisha chanzo kizima , pia tujue ni vifaa gani vya kwenda navyo kwenye kituo husika ili tuchukue sampuli ,neno sampuli humaanisha kiasi kidogo
cha kitu unakichukua kwaajiri ya kufanyia utafiti fulani lakini pindi utakapo pata jibu la kile unachokitafuta basi hiyo sampuli itawakilisha kitu kikubwa , mfano sampuli ya damu ya mnyama inaweza kuwa kiasi kidogo lakini ikawakilisha damu yote ya mwilini labda ikatolewa kwa ajili ya utafiti wa magonjwa, vivyo hivyo ni sawa na maji pia .






2       UCHUKUAJI WA SAMPULI ZA MAJI


 Katika kuchukua sampuli ya maji kunatofautiana kutokana na aina ya chanzo cha maji mfano  jinsi utakavyochukua sampuli ya maji ya mtoni ni tofauti na vile utakavyochukua sampuli ya kisima , pia hata ile ya bombani ,pia kuna chupa maalumu za kubebea sampuli nazo chupa hutofautiana ikitegemea nini kitakachoangaliwa kwenye maji ya chanzo husika mfano utakapo chukua sampili ya maji ili kujua kiwango gani cha hewa ya oxigeni kilichotumiwa na bacteri ili kuvunja vunja vitu vilivyooza ni lazima chupa yake iwe isiyopitisha mwanga wa jua ili kuzuia bacteria wasifanye kazi ndani ya maji hapa sitaelezea jinsi ya kuchukua sampuli ya vyanzo mbali mbali bali itakuwa ni mada itakayojitegemea wakati mwingine , lakini mkazo hapa , ili kupata majibu yaliyo sahii ni vema kuzingatia njia za uchukuaji wa sampuli na si kila mtu anaweza kuchukua sampuli bali ni mafundi sanifu wa maabara au mtu aliyepata mafunzo maalumu , baada ya kuchukua sampuli husika ni vema kukumbuka kufunga vifuniko vya chupa vizuri ili kutoruhusu kitu tofauti cha nje kuingia na pia kwa usalama wa sampuli isije kumwagika wakati wa safari ya kurudi











3       KUBANDIKA LEBO KATIKA KILA SAMPULI


 Ni kitu muhimu sana kubandika lebo katika kila chupa ya sampuli iliyokusanywa , hapa lebo itaonyesha ni muda gani sampuli ilichukuliwa na tarehe , chanzo cha sampuli mto bomba au kisima , jina la mtu aliyechukua sampuli , na mwisho kama sampuli inahitaji kutunzwa kwenye mazingira fulani ili isije kupoteza uhalisia wake











      4.  SAMPULI KUFIKISHWA MAABARA ILI ICHUNGUZWE


Hapa kabla sampuli ya maji haijachunguzwa  lazima isajiliwe , kuwa inatoka wapi , ni aina gani ya chanzo cha sampuli , pia nini kinachotakiwa kichunguzwe kwenye hiyo sampuli


Hapa sampuli ukutana na watu wengine tofauti walioajiriwa kwa kazi hiyo ya kusajiri sampuli na uwenda ikapewa namba ya utambulisho ili majibu yatakapo patikana yapelekwe mahali sampuli ilipotoka ili kuzuia kuchanganywa


Baada ya kusajiliwa kwa sampuli ,ni lazima maabara iwe tayali kwa ajili ya kufanya uchunguzi , hapa lazima wawepo mafundi sanifu ambao watabaki pindi wengine walipoenda kuchukua sampuli ili kuweka maabara katika hari safi na ya usalama ili kufanya kazi , mfano vifaa , vitakavyotumika viwe kwenye usafi na visivyo na matatizo , pia chemikali ziwe zimestandadaiziwa vizuri , sampuli upimwa kwa umakini ilikujua nini kilichomo au kinachokusudiwa , zipo njia mbili kuu zitakazotupa majibu ya kile tunachokitafuta katika maabara , yaani


·   Kutumia vifaa vinavyotoa majibu kidigitari


·   Na ile inayohusisha titresheni ambapo kemikali   huusika sana


Ingawa kwa uchunguzi wa kibailogia huwa tofauti na njia hizo kuu mbili , kwa sababu husisha kuotesha wadudu hivyo majibu upatikana kwa kila sampuli ingawa majibu mengine yanaweza kuchukua siku zaidi ya moja kwa kuwa wadudu wanaoteshwa kwa kupewa chakura Fulani , na katika jotolidi Fulani










5. ULINGANIFU WA MAJIBU NA VIWANGO VYA NCHI HUSIKA AU VYA KIMATAIFA


Baada ya maji kupimwa kitaalamu na kwa umakini mkubwa majibu yatakayopatikana ni lazima yalinganishwe na viwango vya nchi husika au vya WHO yaani kimataifa hii ni kutoka na ukweli kwamba si kila nchi inaweza kufiti viwango vya kimataifa kutokana na hali ya uchumi , ingawa utagundua kuwa viwango vya kimataifa vimejitahidi mno kupunguza athari au madhara yatakayo tokana na kemikali zitakazo onekana katika maji


Ukilinganisha na zile za nchi husika . hivyo baada ya kugundua kuwa maji yamekidhi viwango au la hatua ifuatayo ndio itakayohitimisha zoezi zima.



6. KUTOA RIPOTI



Katika hatua hii , ripoti itaandaliwa baada ya kulinganisha majibu tuliyopata na viwango vilivyowekwa mfano ikatokea kwamba kemikali zilizomo kwenye maji ni nyingi ukilinganisha na viwango vilivyowekwa basi fundi husika atatoa mapendekezo kuwa nini kifanyike , mfano kuweka dawa ili kuondoa lilichokuwemo au kutoa katazo kwamba maji yasitumike kabisa yanaweza kusababisho vifo au matatizo ya mda mrefu , baada ya hapo mteja atapewa majibu yake yenye ushauri jinsi gain afanye kutoka na ain ya maji anayotakakutumia .




Ushauri wangu hapa ni kwamba usitumie maji kwa mazoea , hasa matumizi ya kunywa kwa sababu gharama utakazotumia kujitibia zitakuwa kubwa zaidi kuliko pale utakapofuata ushauri wa wataalamu juu ya matumizi


Unaweza kuniandikia au kuomba ushauri juu ya aina ya maji unayotumia , kusudi lako husika , nami nitakushauri


Lengo la blogu hii ni kutoa elimu , juu ya sayansi ya maji na pia kusaidia jamii juu ya matumizi bora na sahihi ya maji ili yaweze kuwa uhai katika maisha yetu ya kila siku na vizazi vijavyo .









Hakuna maoni:

Chapisha Maoni