Tafuta katika Blogu Hii

Jumapili, 6 Septemba 2015

KUENEA KWA UGONJWA WA KIPINDUPINDU NA MATUMIZI YA MAJI


Hivi karibuni kumeibuka kwa ugonjwa wa kipindupindu katika jiji la Dar es salaam hasa wilaya ya kinondoni ikishika nafasi ya kwanza kwa kuwa na wagonjwa wengi , ugonjwa huu husababishwa na bacteria anayeitwa vibrio  cholerae , bacteria huyu hupatikana kwenye kinyesi cha binadamu , hivyo ili upate ugonjwa huu ni lazima utakuwa umekula kinyesi pasipo kujua pia ugonjwa huu huenezwa na mawakala wa uchafu hapa nazungumzia mdudu anayeitwa nzi ambaye hupenda kusogelea maeneo machafu hasa yenye vinyesi vya wanyama , huwenda ulikula tunda ambalo halikuoshwa ipasavyo au chakula ambacho hakikuhifadhiwa vizuri hivyo nzi mawakala wakatua kwenye chakula na kuacha vimelea vya magonjwa , lakini kikubwa zaidi matumizi ya maji ambayo si salama kwa kunywa , niliwai kutembelea baadhi ya maeneo ya jiji nikiangalia au kukagua ni kipi kisababishi cha ugonjwa huu wa kipindupindu yapo mengi niliyojifunza lakini kikubwa hasa ni swala zima la mazingira machafu katika maeneo ya nayozunguka nyumba za watu au sehemu za kibiashara kama sokoni




 

SABABU ZIFUATAZO ZILINIFANYA KUANDAA MADA HII KAMA KISABABISHI

 

1.Miundombinu mibovu ya mfumo wa maji taka na maji safi

Jambo hili nimewahi kuliongelea sana , miundombinu chakavu ya maji taka usababisha maji taka kukutana na yale yaliyokuwa safi , uwenda ni yale yaliyotibiwa na dawasco au visima vifupi ambapo watu wamekuwa wakitumia maji hayo ya visima vifupi wakijua ni chemichemi kumbe ni kuvilia ndani kwa ndani kwa maji taka lakini hili linaenda sambamba na ukosefu wa vyoo bora katika baadhi ya maeneo , kuna maeneo ukiingia chooni unaweza ukagairi kujisaidia hata kama ungebanwa vipi na haja , vyoo chakavu vilivyofikia hatua ya kutapika ni rafiki kwa nzi wa kijani kubeba vimelea vya magonjwa hasa kipindupindu  

 
 

2. uwepe wa maji taka karibu na makazi ya watu

Kuna maeneo mengi sana katikati ya jiji la Dar es salaam ambapo ni kawaida kukuta maji machafu yakituama kandokando ya makazi ya watu huku kukiwa na shughuli mbalimbali zikiendelea kama huduma ya vyakura maarufu kama mama ntilie ,hii pia ni hatari kwa watoto wadogo ambao wakati mwingine huona maji hayo kama ni sehemu tu ya michezo yao , huenda wasifikie hatua ya kuyatia kinywani lakini uwezekano wa kugusana nayo mikononi ni mkubwa hivyo wazazi nao wasipokuwa makini mtoto anaweza kula kitu kingine bila ya kunawa mikono na kusababisha kupata ugonjwa , sababu hii inaweza kuwa ya msingi kwa sababu takwimu zimeonyesha kuwa miongoni mwa wagonjwa watoto wamekuwa wengi ukilinganisha na idadi ya watu wazima

 

3 .watu kutozingatia kanuni za afya asa usafi binafsi , mfano kula chakula bila kunawa vizuri , kunywa maji yasiyotibiwa au kuchemshwa , pia kama nilivyosema kuhusu watoto ambao awapatiwi uangalizi wa kutosha kutoka kwa wazazi wanapokuwa katika michezo au katika maswala mazima ya ulaji

 

4. mkusanyiko mkubwa wa watu katika eneo moja ,

Hapa ndipo chanzo cha ugonjwa , kukua kwa kasi kwani utagundua nyumba moja ya kupangisha inaweza kuwa na watu wengi au kukaribiana bila nafasi kati ya nyumba na nyumba hivyo unaweza kuona maeneo hayo maarufu kama uswailini , wakati mwingine uwezi kutofautisha kuwa choo Fulani ni cha nyumba hipi , mifumo ya maji taka mara zingine huingiliana kati ya nyumba na nyumba  kiasi kwamba tabia za baadhi ya watu kutozingatia kanuni za afya upelekea kupatwa na ugonjwa , lakini kwa sababu watu wamekusanyika eneo moja ni rahisi sana kwao kuambukizana , hivyo ni vizuri watu wakajaribu kuishi katka maeneo yenyempangilio wa makazi bora unaoleta maana ya kuishi , mfano mzuri ni wilaya ya ilala ambapo si mara chache sana hupatwa na kipindupindu ,ingawa pia yapo maeneo hatarishi lakini maeneo mengi yamepangilika kimakazi  

 

NINI KIFANYIKE KATIKA KUKABILIANA NA UGONJWA HUU HATARI

Katika kutatua au kupambana na tatizo hili kiuna makundi ya kijamii mashirika binafsi na serikali

1 kijamii

   Swala la usafi wa mazingira linaanza na mtu mmoja mmoja , hasa katika ngazi ya kifamilia , tuache kuwa wavivu wa kukemea au kusemana kuhusu usafi katika maeneo yetu tunayoishi , pia tuache dhana ya kuilaumu serikali bila kufanya sehemu yetu, kama mwanajamii tunawajibu wa kulinda miundombinu ya maji , wapo watu hukata kwa makusudi mipira ya kusambazia maji safi ili ajinufaishe wao , si gharama pekee itakayoingia serikali kufanya matengenezo bali itapelekea kuingiliana kwa mifumo ya maji safi nay ale ya maji taka

 

2 serikali au sekta zisizo rasimi nazo zinaweza kuchangia kuenea kwa ugonjwa kwa namna moja au nyingine , mfano yapo maeneo ambapo hakuna ufatiliaji juu ya miundombinu chakavu inayopitisha maji safi na maji taka ili kujua wapi kuna mipasuko inayo sababisha maji yawe na vimelea vya ugonjwa , hivyo sampuli za maji zichunguzwe kila baada ya mda Fulani kujua kama kuna uchafuzi wa maji au la

Pia mamlaka husika kama wizara ya afya inajukumu kubwa la kuhakikisha elimu ya kutosha inawafikia watu ili wawe na mitazamo mizuri kuelekea afya na mazingira yao.

 

Jumapili, 16 Agosti 2015

CHANGAMOTO ZA MAJI TAKA KATIKA MAJIJI YANAYOKUWA


MAJI TAKA

Maji taka ni yale maji yaliyogusana na uchafu au kitu kisichohitajika kwenye maji , yakihusisha mkusanyiko kutoka mahali tofauti tofauti mfano nyumbani , maji yaliyotumika kuogea ,kufulia , kuoshea viombo na wakati mwingine yakihusishwa na uwepo wa vinyesi , pia maji haya yanaweza kutoka viwandani au kwenye taasisi mbalimbali .

Mkusanyiko wote wa maji haya taka hukutana katika bomba moja kubwa ambalo litasafilisha kuelekea kwenye kumwagwa au kusafishwa na kutibiwa ili yawe katika kiwango kisicholeta madhara kwenye mazingira

Kumekuwapo na changamoto juu ya haya maji taka hasa sehemu za  mijini,uwenda hata wewe ukawa mmojawapo kati ya wale waliokutana na kero ya kuona au hata kukanyaga maji haya machafu wakati ukiwa katika matembezi ,

Maji haya taka ni hatari hasa pale yanapokutana na mfumo wa maji safi ,ambapo  mipira ya kusambazia maji safi inaweza kupasuka hivyo ikapelekea athari kubwa kwa watumiaji    


 

SABABU ZA MAJI TAKA KULETA KELO MIJINI

Hapa kuna sababu nyingi zinazosababisha tatizo hili sahemu za mijini ingawa wapo wanasiasa wanaodai kuwa inatokana na ujenzi unaondelea kila kukicha katika miji mikubwa hasa ujenzi wa majengo marefu , sitaki kusema sio kweli lakini kuna ukweli kwa kiasi Fulani kwa sababu niliwahi kushuhudia binafsi eneo moja muhimu sana la serikali siwezi kulitaja na najua yapo maeneo mengi kama hayo ambapo mvua iliponyesha nilishangaa kuona maji yakituama eneo moja na hata kusababisha ofisi niliyokuwa nafanya kazi kuingiliwa na maji , nilitafiti ili nijue hasa tatizo liko wapi , ndipo ilionekana wazi kuna chemba iliyokuwa inapitisha maji taka kuzibwa makusudi ili kuruhusu ujenzi wa majengo hayo ya serikari . Ilinisikitisha sana kama mtaalamu husika wa maji na miundombinu yake na hivyo ndivyo ilivyo katika maeneo mengi na sio sababu kubwa inayoweza kunishawishi kwa sababu ujenzi ukizingatia miundombinu bora ya maji badala ya kujenga ilimradi tatizo la maji taka mijini litapungua au kwisha kabisa.

 Sababu zifuatazo zitatuonyesha jibu la msingi na amini usiamini ndivyo ilivyo

1 . Ongezeko la watu sehemu za mijini

Watu wengi wanapojazana sehemu moja wakiwa katika utafutaji hivyo matumizi ya maji yanakuwa makubwa na maji taka kuwa mengi hii upelekea miundo mbinu hiyo kuelemewa na kiwango cha taka  au maji yanayosafirishwa

 

2. Utupaji taka ovyo

Kila mtu anafahamu yakuwa majiji makubwa yana kabiliana na changamoto kubwa ya uchafu kutokana na mamlaka husika kutowajibika ipasavyo katika utatuzi wa tatizo la uchafu hasa jiji letu la Dar es salaam , swala hili pia huendana na tabia mbaya ya mazoea ya baadhi ya  watu kutupa taka kama za plastiki ovyo , taka hizi husababisha zile chemba muhimu za kupitisha  maji taka kuziba na hivyo maji yanaposhindwa kupita njia iliyopangwa yatatafuta njia mbadala ili yaendelee na safari , hivyo ndivyo watumia barabara na watu wenye shughuri zao mijini wanakutana na kelo ya maji machafu.
3. Uchakavu wa miundo mbinu
   Inawezekana kabisa kuna wakati Fulani miundombinu inayo ruhusu maji taka kupita inatakiwa kufanyiwa matengenezo au kubadili vifaa vya zamani na kuweka vilivyo kuwa vipya ilkusaida mfumo endelevu

NINI KIFANYIKE KATIKA KUTATUA TATIZO HILI ?

Njia zifuatazo ni muhimu katia kushughulika na tatizo

1.Kuwe na ujenzi bora utakao zingatia upitishwaji wa maji safi na maji taka

 Hii itasaidia majitaka kusafiri katika njia zake na hata mafuliko yatakapotokea kusiwe na athari itakayojitokeza maana mifumo husika itaruhusu maji yasituame . ujenzi pia utaenda sambamba na ongezeko la watu , hii ni hesabu za takwimu kwamba miundo mbinu itaweza kubeba maji taka kwa miaka mingi zaidi ikilinganishwa na ongezeko la watu kila mwaka

 

2. Mamlaka maalumu pia izingatie swala la usafi ili kuepisha kuziba kwa chemba za maji taka

Chombo kilichopewa dhamana ya usafi katika majiji makubwa kihakikishe kina weka vifaa maalumu vya kutunzia taka hasa sehemu za mikusanyiko ya watu , cha ajabu unaweza ukatembelea vituo vya dara dara hasa Dar es salaama na usikutane na kitunza uchafu hata kimoja , hii umfanya mtu aliye na taka mkononi kutupa ovyo , jambo hili pia liende sambamba na elimu juu ya usafi , hapa kila mmoja anawajibika kumueleza mwenzake juu ya utunzaji wa mazingira

 

3. kadri inavyowezekana katika taasisi mbali mbali kuwe na mifumo ya ndani ya kutibu maji taka badara ya kusafiri umbali mrefu kwa ajili ya kutibiwa , hii inaweza pia kupunguza gharama na pia inaweza kuzuia kukutana kwa mfumo wa maji taka na ule wa maji safi .mfano wa mifumo ya ndani ni kama pondi za maji taka ,  
 
Asante karibu tena kwa mada nyingine nzuri za kukufanya ubadilike juu ya mazingira na hasa matumizi ya maji

 

 

 

 

Jumapili, 9 Agosti 2015

FAHAMU KUHUSU ALGAE FLOC


Ni dawa inayotumika katika sayansi ya kutibu maji , iliyotengenezwa kutokana na vijidudu vinavyoitwa algae ,algae ni miongoni mwa viumbe hai vyenye ukijani kama majani

Wakati maji yamepitia njia tofauti tofauti ya usafishwaji    .Kazi moja kubwa ya algae floc ni kusafisha maji ambayo yamejumuisha taka ndogo sana ambazo zilifanikiwa kupenya kupitia kwenye machujio , taka zote zenye umbo dogo hukusanywa na algaefloc mbayo hutokeza mabonge ambayo mwisho huzama chini kwa nguvu ya mvutano tayari kuondolewa nje ya tanki kwenda kutupwa kama uchafu

Jumapili, 2 Agosti 2015

FAHAMU NJIA BORA ZA MATUMIZI YA MAJI ILI KUPUNGUZA GHARAMA YA KULIPIA


Tunaishi kwenye dunia ambayo kila kitu ni gharama ,hasa yale mahitaji ya msingi ya mwanadamu ikiwemo maji mahitaji yote haya mwisho wa siku yanatugharimu pesa kutokana na thamani ya tulichotumia hivyo ni vema kuwa na utaratibu mzuri wa matumizi ili kupunguza gharama  

 

Nitaelezea njia zifuatazo zitasaidia kabisa kupunguza gharama kama ukizifuata kwa makini

 

 


1.kuwa na mita ya kujua kuwa ni kiasi gani cha maji ulitumia kwa mwezi mzima

Mita za maji ni jambo la kawaida kwa watu wanaonunua maji kutoka kwa watu binafsi au mamlaka husika za kiserikali ,lakini kama wewe ni muuzaji wa maji uliye na kisima chako acha kuwa na biashara ya mazoea nunua mita ili ikusaidie kujua unauza maji ya kiasi gani kila mwezi , rekodi katika kitabu au mahali popote jumla ya kiwango cha maji ulichotumia kwa mwezi mzima fanya hivi kila mwezi bila kuacha hii itakupa picha harisi juu ya maji unayotumia mara kwa mara  

 

 

2.Orodhesha maji unayotumia kwa makusudio gani , kuoga ,kufulia nguo , kunywa kusafishia choo au sehemu mbali mbali za nyumba, umwagiliaji au kuuza , orodha hiyo itakusaidia  kufahamu ni maeneo gani ambayo maji yako yanatumika sana na je kuna unuhimu gani wa hilo eneo maji yakatumika sana , mfano ukipanga au kuishi kwenye nyumba ambayo hutumia vyoo vinavyohitaji maji mengi ili kusukuma kinyesi hauna jinsi inaweza kugharimu sana matumizi ya maji hivyo hakikisha unatumia aina ya choo ambacho hakihitaji maji mengi kama eneo unaloishi lina tatizo la ukosefu wa maji lakini ukijua kuwa maji yanatumika sana kuoshea au kufulia unaweza kudhibiti au kupunguza matumizi



3.Hepuka kwenda kwenye bomba la maji mara kwa mara

Kuna watu kwa sababu tu wameona kuna bomba linatiririsha maji basi hufungulia kila wakati labda chombo kimoja au viwili vimechafuka basi mtu ataenda kusafisha huku akiruhusu maji , ni vizuri kuweka utaratibu wa kuosha viombo kwa ujumla wake , au badala ya kila siku kufua nguo moja au mbili ni vizuri kupanga siku maarumu kwa ajili ya kufua nguo nyingi mbazo utavaa hata zaidi ya wiki moja 

 

 

4. Kemea na kisha toa elimu kwa wanafamilia au watumiaji wenza wa maji pale uzembe wa kuruhusu maji yatoke bila mpango au kwa kujisahau ili watambue utaratibu utakao jiwekea , kila mmoja anapaswa aelewe juu ya umuhimu wa kutumia maji kwa utaratibu ili kuepusha gharama za ulipaji

 

5. Furahia kulipia maji kwa wakati ili kuepuka usumbufu wa kukatiwa

Unapolipi maji kwa wakati itakusahidia kufurahia thamani ya ulichokilipia mbali na kulimbikiza unaweza kujenga hisia baadae kuwa utapaswa kilipia usichostahiri kisha utasema mita imeenda sana na maji yametumika kidogo    

 

Jumapili, 26 Julai 2015

REVERSE OSMOSIS

RO huondoa chembe ndogo ndogo za uchafu pale maji yanayosafishwa hupita katika kiwambo chembamba ambachokinaweza kuruhusu maji yakiwa pekeyake bila uchafu

Kinachotoke ni kwamba maji ambayo yana kiwango Fulani cha chumvi au madini mengine  husukumwa na msukumo mkali kupita kwenye kiwambo chembamba hivyo msukumo hupungua pale yanapo toka yakiwa katika hali bora

Vifaa vya RO huwa na uwezo wa kufanya kazi katika msukumo  wa kati ya 200  -  800 psig

 

Pia RO imetengenezwa kiasi kwamba maji yanatibiwa dhidi ya bacteria  kwa kutumia mionzi ya uv ingawa pia kiwambo chembamba kinachoruhusu maji yasiyo na chumvi iliyoyeyuka kupenya ina vitundu ambavyo vinaweza kutoruhusu bacteria kupenya hivyo wakaondolewa kwa njia ya kawaida
 
JINSI RO INAVYOFANYA KAZI

Mada iliyopita nilielezea maana ya RO hivyo hapa nitaelezea jinsi gani mtambo huu ufanya kazi , lengo langu ni kwamba msomaji wa blogu hii upate kuelewa kwa namna Fulani juu ya RO

Maji kutoka kwenye chanzo huingia kwenye maifazio na kisha kuruhusiwa kwenda kwenye mtambo ili kazi ya kusafishwa iweze kuanza  kitendo cha asili yaani osmosis huitaji maji yaliyo katika msukumo mdogo kwenda kwenye yale yaliyo na msukumo mkubwa yakipita kwenye kiwambo chembamba cha matilio maalumu ya kuchuja 

Neno reverse humanisha  kinyume hivyo kifaa hiki  uruhusu maji yenye mgandamizo mkubwa kwenda mdogo kwa msaada wa pampu ambayo usaidia katika msukumo na hivyo ndivyo maji yanapochujwa hivyo maji yenye mgandamizo mkubwa huelekea kwenye eneo lenye mgandamizo mdogo  hivyo msukumo mkubwa ndio utakao sababisha chumvi iliyoyeyuka iweze kuondolewa kwa kiwango kikubwa , wataalamu huamini kuwa RO inaweza kuondoa asilimia 95 hadi 99 za chumvi iliyoyeyuka

 

Pia ufanisi unapoonekana umepungua tatizo linaweza kuwa viwambo vyembamba vikawa vimezidiwa uwezo wa kuchuja au kuondoa chumvi iliyoyeyuka hivyo huitajika vibadilishwe

 

Jumapili, 12 Julai 2015

REVERSE OSMOSIS


RO ni kifaa cha kisasa kinachotumika kuondoa chumvichumvi ambayo hutokeza maji magumu  , mada zilizopita nilielezea madhara ya maji magumu

Kifaa hiki kimetengenezwa kiasi kwambwa kina uwezo wa kuvuta chuvi chumvi yote na kuyaacha maji yakiwa salama

Lakini  uwezo wa kuondoa chumvi hutofautiana kwa kifaa kimoja na kingine ikitegemeana na kiwango cha chumvi

Pia RO imetengenezwa kiasi kwamba maji yanatibiwa dhidi ya bacteria  kwa kutumia mionzi ya uv

 

 

Jumapili, 5 Julai 2015

JE KILA MTU ANAWEZA KUSAFISHA MAJI YA KISIMA AU BOMBA LAKE ?


Kama ilivyo leo kuna madaktari wengi ambao wamefungua vituo kwa ajili ya kutoa huduma za afya kwa jamii lakini si madaktari wote wamekidhi vigezo na masharti kwanza vya wao kuwa madaktari waliosomea fani hiyo ipasavyo na pili huduma wanayoitoa kwa wateja wao , kuibuka kwa wimbi la madaktari feki limekuwa tatizo kwenye sekta ya afya kwani wengi kwanza wamekuwa na gharama kubwa za matibabu kwa wateja na pia wakati mwingine kutoa maelezo yasiyo ya kweli kwa wagonjwa , pamoja ya kuwa kuna fulsa ya kujiongezea kipato kwa mtu kuwa na kituo chake cha huduma za afya lakini taaruma ni vema izingatiwe kuliko kujali pesa , vivyo hivyo ata kwenye suala la ubora wa maji lina taka ueledi na utaalamu ili kulinda afya za watu , nakumbuka wakati tuliokuwepo chuoni kimasomo mwalimu wetu aliyetufundisha somo la kutibu maji alituambia kuwa kama fundi sanifu katika maabara ya maji lazima uwe makini katika kuzingatia kiwango cha dawa kinachohitajika kwenye maji ili kupambana na vijidudu , alisema kuwa fundi sanifu anaweza kuua watu wengi kwa mda mfupi kuliko hata mwanajeshi anayetumia silaha vitani.
 




 

Mada hii nimeonelea ni vema nichapishe kwa sababu kuna mtu alishawahii kuja kuniuliza kuwa yeye maji yake ni machafu yakiwa na rangi inayoashiria uwepo wa madini ya chuma kwa wingi na turbidity(chembechembe ndogo za viasili vya kioganiki na vile visivyo vya kioganiki ) hivyo akaniambia kuwa aliwahi kununua shabu ikiwa kama mawe bila shaka ni aluminiam sulfate ili kuyasafisha maji hivyo alikuwa na nia ya kuweka ili asafishe kisima chake alitamani asikie sauti yamgu kama ningemluhusu aweke,  hapa ndipo lile swali ya kwamba kila mtu anaweza kusafisha maji yake linapopata jibu ya kwamba si kweli  hataukipewa kemikaliya klorini uweke kwenye maji ili kuua vijidudu haitashangaza kusikia umeua watu kwa sababu ya kutokuwa na utaalamu juu ya maji , hivyo lazime tuheshimu taaruma kuliko kujichukulia hatua mkononi binafsi naheshimu ninaposikia kuwa mtu katumia miaka kadhaa kusomea taaruma Fulani mfano nafahamu kuwa nikiumwa kichwa kuna dawa za kutuliza maumivu lakini unapokutana na daktari aliyetumia muda wake mwingi akiwa shuleni kusomea magonjwa ya mwanadamu huenda akaniambia tu wala nisitumie dawa ya kutuliza maumivu bali ninywe maji kwa wingi hivyo kichwa kitapona

 

HIVI NDIVYO UNAVYOTAKIWA KUFANYA MAJI YAKO YANAPOKUWA MACHAFU NA UKAHITAJI KUSAFISHA ILI KUUZA AU KWA MATUMIZI TU YA NYUMBANI

 

Nilimwambia mteja kuwa usijalibu kamwe kuweka hiyo dawa kwenye maji bali alitakiwa kuwaona mamlaka husika yaani wizara ya maji na mamlaka zinazotambulika hivyo lazima wangemwambia ni lazima sampuli ya maji yake ichukuliwe na kupelekwa maabara iliifanyiwe uchunguzi , pia angeambiwa na gharama ya kupima maji yake , na endapo taratibu zote zikifuatwa basi majibu yake yangekuja na ushauri nini kifanyike ili kuyafanya maji yake yawe salama na safi kwa matumizi

Njia hizo nimewahi kuzieleza kwenye mada inayosema  JINSI YA KUJUA MAJI NI SAFI NA SALAMA KWA MATUMIZI unaweza kuisoma na ukafahamu jinsi wataalamu watakavyo kusaidia

Endapo kama unahitaji maoni au ushauri juu ya maji unayotumia unaweza kunitumia barua pepe katika  mackthekwembe@gmail.com    

 

 

Jumapili, 28 Juni 2015


Maji yaonekanavyo inaweza kuchukuliwa kuwa hakuna shida au madhara yatokanayo lakini , madhara yake ni makubwa pale madini ya chumvi chumvi yanapo fanikiwa kuingia kwenye  mitungi ya machemshio   kiasi kwamba kiwanda kinawaza kufungwa  au ikagharimu pesa nyingi kuhakikisha uzalishaji unaendelea . 

Mitungi mikubwa ya kupozea au kuchemshia  hupatwa na athari za maji magumu pasipo kuangalia ubora wa hayo maji yanayotumika wakati wote hivyo ni jambo lisilohepukika


MADHARA YATAKAYOJITOKEZA PALE MAJI YENYE UGUMU  YATAKAPO TUMIKA KWENYE MACHEMSHIO

Pia maji ambayo hutumika kutengenezea au kuchanganyia dawa au kemikali kwa ajili ya kuzuia tatizo yanaweza kuchangia tatizo kama hhayaja safishwa vema

Kwa sababu maji yenye  ugumu hutokana na chumvi chumvi pale yanapotumika pasipo uangalifu hivyo ni vizuri kuwekeza kwenye teknologia ya maabara ya maji itakayosaidia kujua muonekano au ubora wa maji kabla hayajatumika  na yafuatayo ni madhara

  

Ca(HCO3)       +  JOTO              —›          H2O    +  CO2 (gesi)    +  CaCO3(Chanzo cha maji magumu au yenye chumvi chumvi)

 
 
 
 
 
 
 

kielelezo hapo juu ndio mfano halisi wa kile kinachotokea kwenye machemshio

 kalisiam kaboneti ndio mgando mgando unaojibandika kwenye kuta za machemshio na hivyo usababisha joto liwe kali sana kuliko inavyotakiwa lakini pia itakapotoke joto likazidi kupita kiasi machemshio yatakuwa mbioni kubutuka

 
Lakini pia majimagumu yatakapoachwa bila kutibiwa yatasababisha tabia ya kuzua joto lisisambae  maeneo yote ya machemshio


Tatizo lisipopatiwa ufumbuzi inaweza kuzuia ufanisi mzima wa mitungi ya kuchemshia  

 

NJIA ZA KUONDOA MAJI MAGUMU KABLA HAYAJALETA MADHARA

Kuna njia mbalmbali  za kuondoa chumvi chumvi za maji magumu  , nji ya kwanza ni kutumi kifaa kinachoitwa softener ambacho kina uwezo mkubwa wa kuondoa hizo chumvichumvi lakini kinatumika pale kabla maji hayajaingia kwenye mitungi ya kuchemshia

Mbali na softener tunaweza pia kutumia RO au reverse osmosis  ambapo kifaa hicho nacho huondoa kiasi kikubwa cha chumvi chumvi na kuzuia athari kabla ya maji kuingia kwenye mtungi wa kuchemshia

 

Njia nyingine ni kutumia chemikali ambazo zina phosphate au kaboneti ndani , polymers kama vile ctalized silphate  

 

Kama kuna jambo la kiteknolojia unaweza kuniandikia au kunitumia email ambayo ipo kwenye hii blogi

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Jumapili, 21 Juni 2015

FAHAMU KUHUSU TDS KATIKA MAJI


                                                            
TDS  ni neno linalotumika kama msamiati na kifupisho cha maneno ya kiingereza yanayojulikana kama Total dissolved solids  ikimaanisha kuwa ndani ya maji ambayo yamekutana au kugusana na viwakilishi mbali mbali kama vya kiumbo , kikemikali au vya kibaiologia  hivyo TDS , huwakilisha mgusano wa maji na chembe chembe za uchafu zikijumuisha element au kompaundi mbalimbali za kikemikali zilizoweza kuyeyushwa na maji au zilizotengeneza mgando mgando kutokana maji kushindwa kuziyeyusha , hivyo basi chembendogo hizo zinakuwa na chaji chanya na hasi   pia TDS hujumuisha hata chumvi zisizokuwa za kioganiki

 
 

 

TDS hutuonyesha picha ya kwamba ni jinsi gani maji yetu yamechafuka au kukutana na uchafu ingawa ni ngumu kutupa jibu halisi la kiwango cha uchafuzi  hasa katika maji ya kunywa  hivyo mara nyingi tunapokuwatunapima mahabara  TDS hutupa picha ya kwamba majibu ya vipimo vingine yatakuwaje mfano TDS inapokuwa kubwa tunategemea pia chloraidi iwepo .

Kiwango kilichowekwa na EPA huko marekanni kuhusu TDS inatakiwa kisizidi milligram 500 katika lita yamaji                     

 

 

 

                                                           JINSI YA KUPIMA TDS KATIKA MAJI

Kwa sababu TDS hujumuisha chembechembe ndogo zilizo na chagi hasi na chanya hivyo huwa zinatembea zikigongana kwenye maji kila moja ambapo kitaalamu huita ions kwa jinsi hiyo njia ya kielekroniki hutumika katika kupima hizo chembe chembe zilizobeba chagi 
TDS hupimwa katika miligramu kwa lita moja (mg/l)
Wataalamu wametengeneza kifaa kinachoitwa TDS – Meter  ambacho hutumika katika kupimia

Kifaa hicho kimetengenezwa kiasi kwamba huwa na uwezo wa kuhisi kuwa kuna kiwango gani cha TDS lakini pia kuna mahusiano ya karibu sana kati ya TDS pamoja na EC neno EC hutokana na neno la kiingereza yaani electric conductivity ambapo humaanisha uwezo wa maji yenye chembechembe hasi na chanya kupitisha umeme huwezo huo upimwa katika microsemens per sentimita

 

Kifaa kwa ajili ya kupima TDS kimetengenezwa kuwa na uwezo wa kupima na EC pia . ingawa kinaweza kusomwa katika mtindo wa skeli au wa digitali ikitegemeana na watengenezaji wa kifaa husika walivyotengenezwa  , kifaa pia huwa na mahari penye kihisia  ambapo kiasi kidogo cha sampuli ya maji humiminwa ili kujua kiwango cha TDS na EC






 












Sampuli ya maji inaweza kutibiwa kwanza kabla ya kupima ikitegemea ni aina gani ya sampuli pia kifaa ni lazima kikaguliwe kama kipo katika ubora wake

Baada ya kukagua kifaa , kuwa kipo tayali kiasi kidogo cha sampuli kitamiminwa kwenye kifaa na kubonyeza kitufe cha kupimia ndipo jibu litaonekana katika mfumo wa digitari au wa skeli  ,

 

 

 

      

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

  

 

 

 

Jumapili, 14 Juni 2015

MAJI MAGUMU ( HARD WATER)


 

 Maji magumu ni maji ambayo yanapotumika kuoshea viombo au kufulia nguo hayawezi kutokeza povu , bali utaona utando mweupe ukielea juu , je hii usababishwa na nini ?

Maji magumu huwa yanakuwa na kiasi kikubwa cha madini ya chokaa, yanayotokana na metali za kalishamu na magniziamu , metali hizo uyeyushwa pale maji yanayotokana na mvua kupenya chini ya ardhi ambapo miamba yenye nyufa uruhusu maji yasiyo na madini kwenda kuyeyusha metali za chokaa na kusababisha maji yawe magumu

 
 

Maji haya yanaweza kuwa mahari popote ambapo kuna miamba yenye madini ya chokaa , yaani kalisiam kaboneti au magniziam kaboneti

 caco2(s)
 
 
 

MADHARA YA MAJI MAGUMU KWA WATUMIAJI
 
Maji magumu hayana madhara katika mwili wa mnyama au mwanadamu pindi atakapo yatumia maji hayo bali athari zake huwa ni kubwa zaidi kwenye viwanda ambapo bilakuwa makini na maji magumu . yanaweza kusababisha hasara kubwa inayotokana na kualibika kwa mitambo hiyo , pia maji magumu usababisha mitungi ya kuchemshia maji isiwe na kiwango kizuri cha kuhifadhi joto , athari huwa ni kubwa ata katika mitungi ya maji kwa ajiri ya kupozea  mitambo ,kutokana na utando mnene wa chokaa kujibandika kwenye kuta za mtambo uliotengenezwa na madini ya metali . .

 

 

 

 

      

Jumapili, 24 Mei 2015

FAHAMU KUHUSU ‘PH” YA MAJI



                                              
  Watu wengi ujiuliza kwamba

PH ya maji ni nini  ?



PH ya maji ni neno la kikemia  hutumika kuwakilisha kupimo  cha asidiki au ukakasi kilichomo kwenye   maji ambapo kiasi hicho cha asidiki au ukakasi upimwa katika mfumo wa ayani zilizokuwa huru kwenye maji, nazo ni haidrogeni  ayani na zile za haidroksaidi ayani 





JINSI YA KUPIMA PH YA MAJI

1.PH ya maji inaweza kupimwa kwa kutumia kifaa maalumu cha kielekroniki kinachoitwa PH-mita  , kifaa hiki kina umbo dogo kiasi kwamba fundi sanifu anaweza kwenda nacho kwenye kituo cha kuchukulia sampuli na akaweza kupima akiwa huko .

















TAHADHARI KATIKA MATUMIZI YA KIFAA

Kifaa hiki ili kitoe majibu sahii ni lazima kikaguliwe kabla ya kutumika , watengenezaji wa kifaa hutoa kumbukumbu muhimu juu ya kifaa zitakazomsaidia fundi sanifu kukikagu juu ya usahii wake .



Kifaa hutumia kitambuzi ambacho ni elekrodi ili kupima kiwango cha ayani kwenye sampuli ya maji , hivyo ni muhimu kukikagua na kukisafisha kila baada ya matumizi lakini mfano wa kitu laini hutumika kusafishia elektrodi ili iwe katika hali ya kuhisi .  

PH- mita ,huifadhiwa kwenye kikasha maalumu kila baada ya kumaliza kukitumia



2. Universal solution . Hii ni chupa kubwa yenye  kemikali maalumu inayotumika kupima ph ya maji ikiwa na lebo inayonyesha rangi tofauti zilizopimwa katika kiwango fulani cha ph ikianzia 0 mbaka 14, kiwango cha vitone viwili  hudondoshwa kwenye kiasi cha mililita kumi hivi za sampuli ya maji, kisha rangi ubadilika kuendana na sampuli ya maji

ipo kwenye kiasi Fulani cha ph kwa kulinganisha na rangi zilizopo kwenye lebo ya universal solution .

  












Pia unaweza kupima PH kwa kutumia karatasi ndogo zinazopima PH ya 0 hadi 14 au inayoishia kwenye 12 , vikalatasi hivi huwa kwenye viboxi vidogo maalumu ambapo uchovywa kwenye
kiasi Fulani cha sampuli na kisha kulinganisha rangi iliyopangwa kitaalamu na ile ilyotokea .








Kwa nini tunahitaji kujua PH ya maji ?


Ni muhimu sana kujua pH ya maji kwasababu itatuambia kuwa nini kimezidi au kimepungua kati ya hali ya uasidi wa maji na hali ya ukakasi wa maji , mfano kwenye  maeneo ambayo maji ya kunywa yanayowekwa kemikali ya klorini ni muhimu kujua ph ya maji ambayo kiwango chake huwa kati 6.5—9.0 , kwa sababu maji hayo yanakuwa na visababishi vyote vya kupanda au kushuka kwa kiwango cha PH


Pia kuna kemikali mbali mbali zinazotumika kuzuia michubuko au kujibandikiza kwa solidi za kioganiki kwenye viwanda mabapo wana machemshio au vipoza mitambo ambapo maji yakiwa kwenye ph Fulani kemikali  hizo haziwezi kufanya kazi ipasavyo au ili tujue zimefanya kazi basi PH iwe katika kiwango fulani


PH ya maji ni miongoni mwa viwakilishi muhimu sana kuangalia kwenye maji , ikiwa unahitaji msaada wa kishauli usikose kunitumia barua pepe yangu yani mackthekwembe@gmail.com  au simu yangu ya mkononi kwa namba 0718746644 



Jumapili, 17 Mei 2015

JINSI YA KUJUA MAJI NI SAFI NA SALAMA KWA MATUMIZI





Unapotaka kujua kuwa maji yako yanafaa au hayafai kwa matumizi lazime kuzingatia kuwa ni nini kusudi la kutumia maji yako .Je ni kwa ajiri ya kunywa na matumizi ya nyumbani , kwa ajiri ya ujenzi , au kwa ajiri ya mapuli ya kuogela ?


Maji kabla hayajatua katika gamba la juu la dunia yakiwa kama mvua yanakuwa katika usalama ila pale yanapoifikia tu ardhi ndipo uhakika wa usalama wake ni sifuri , hii ni kwa sababu kuna mgusano wa mambo mengi ambayo yapo ardhini na maji yanapoifikia ardhi , mfano kuna madini mbali mbali kama vile aluminiam ,calcium na chembechembe za kioganiki , bila kusahau bacteria mbalimbali , ambao ukaa kwenye vinyesi vya wanyama damu moto mfano vibrio cholera . lakini ni mara ngapi tumewahi kuhisi au kuamini kuwa maji ya chanzo Fulani kama chemichemi ni safi na salama na wakati mwingine tumejalibu kunywa bila hata kuchemsha ?  hasa sehemu za vijijini watu wengi wamekuwa wakiishi kwa mazoea , hii imefanya ata kinga zao kukubaliana na mazingira ya maji wanayo yatumia , bila kuhisi kuumwa kwa muda mrefu , lakini angalizo ni kwamba , watu hao wapo kwenye hatari ya kuugua magonjwa yanayotokana na maji kama vile kipindupindu



Je tutajuaje sasa kuwa maji tunayoyatumia ni safi na salama ?

Hapa nitaelezea hatua za awali mbaka ile ya mwisho ambayo itatupatia hitimisho 



1 KUFAHAMU CHANZO CHA MAJI HUSIKA


Chanzo gani ambacho kina maji yanayotumiwa , chanzo kinaweza kuwa mto , ziwa au bwawa la kutengenezwa , kisima ,bomba la maji yakusambazwa au maji ya bahari , lengo la kujua chanzo kinaweza kutupa historia ya eneo husika , lakini kikuubwa zaidi ni ili tupate kuchukua sampuli ambayo itawakilisha chanzo kizima , pia tujue ni vifaa gani vya kwenda navyo kwenye kituo husika ili tuchukue sampuli ,neno sampuli humaanisha kiasi kidogo
cha kitu unakichukua kwaajiri ya kufanyia utafiti fulani lakini pindi utakapo pata jibu la kile unachokitafuta basi hiyo sampuli itawakilisha kitu kikubwa , mfano sampuli ya damu ya mnyama inaweza kuwa kiasi kidogo lakini ikawakilisha damu yote ya mwilini labda ikatolewa kwa ajili ya utafiti wa magonjwa, vivyo hivyo ni sawa na maji pia .






2       UCHUKUAJI WA SAMPULI ZA MAJI


 Katika kuchukua sampuli ya maji kunatofautiana kutokana na aina ya chanzo cha maji mfano  jinsi utakavyochukua sampuli ya maji ya mtoni ni tofauti na vile utakavyochukua sampuli ya kisima , pia hata ile ya bombani ,pia kuna chupa maalumu za kubebea sampuli nazo chupa hutofautiana ikitegemea nini kitakachoangaliwa kwenye maji ya chanzo husika mfano utakapo chukua sampili ya maji ili kujua kiwango gani cha hewa ya oxigeni kilichotumiwa na bacteri ili kuvunja vunja vitu vilivyooza ni lazima chupa yake iwe isiyopitisha mwanga wa jua ili kuzuia bacteria wasifanye kazi ndani ya maji hapa sitaelezea jinsi ya kuchukua sampuli ya vyanzo mbali mbali bali itakuwa ni mada itakayojitegemea wakati mwingine , lakini mkazo hapa , ili kupata majibu yaliyo sahii ni vema kuzingatia njia za uchukuaji wa sampuli na si kila mtu anaweza kuchukua sampuli bali ni mafundi sanifu wa maabara au mtu aliyepata mafunzo maalumu , baada ya kuchukua sampuli husika ni vema kukumbuka kufunga vifuniko vya chupa vizuri ili kutoruhusu kitu tofauti cha nje kuingia na pia kwa usalama wa sampuli isije kumwagika wakati wa safari ya kurudi











3       KUBANDIKA LEBO KATIKA KILA SAMPULI


 Ni kitu muhimu sana kubandika lebo katika kila chupa ya sampuli iliyokusanywa , hapa lebo itaonyesha ni muda gani sampuli ilichukuliwa na tarehe , chanzo cha sampuli mto bomba au kisima , jina la mtu aliyechukua sampuli , na mwisho kama sampuli inahitaji kutunzwa kwenye mazingira fulani ili isije kupoteza uhalisia wake











      4.  SAMPULI KUFIKISHWA MAABARA ILI ICHUNGUZWE


Hapa kabla sampuli ya maji haijachunguzwa  lazima isajiliwe , kuwa inatoka wapi , ni aina gani ya chanzo cha sampuli , pia nini kinachotakiwa kichunguzwe kwenye hiyo sampuli


Hapa sampuli ukutana na watu wengine tofauti walioajiriwa kwa kazi hiyo ya kusajiri sampuli na uwenda ikapewa namba ya utambulisho ili majibu yatakapo patikana yapelekwe mahali sampuli ilipotoka ili kuzuia kuchanganywa


Baada ya kusajiliwa kwa sampuli ,ni lazima maabara iwe tayali kwa ajili ya kufanya uchunguzi , hapa lazima wawepo mafundi sanifu ambao watabaki pindi wengine walipoenda kuchukua sampuli ili kuweka maabara katika hari safi na ya usalama ili kufanya kazi , mfano vifaa , vitakavyotumika viwe kwenye usafi na visivyo na matatizo , pia chemikali ziwe zimestandadaiziwa vizuri , sampuli upimwa kwa umakini ilikujua nini kilichomo au kinachokusudiwa , zipo njia mbili kuu zitakazotupa majibu ya kile tunachokitafuta katika maabara , yaani


·   Kutumia vifaa vinavyotoa majibu kidigitari


·   Na ile inayohusisha titresheni ambapo kemikali   huusika sana


Ingawa kwa uchunguzi wa kibailogia huwa tofauti na njia hizo kuu mbili , kwa sababu husisha kuotesha wadudu hivyo majibu upatikana kwa kila sampuli ingawa majibu mengine yanaweza kuchukua siku zaidi ya moja kwa kuwa wadudu wanaoteshwa kwa kupewa chakura Fulani , na katika jotolidi Fulani










5. ULINGANIFU WA MAJIBU NA VIWANGO VYA NCHI HUSIKA AU VYA KIMATAIFA


Baada ya maji kupimwa kitaalamu na kwa umakini mkubwa majibu yatakayopatikana ni lazima yalinganishwe na viwango vya nchi husika au vya WHO yaani kimataifa hii ni kutoka na ukweli kwamba si kila nchi inaweza kufiti viwango vya kimataifa kutokana na hali ya uchumi , ingawa utagundua kuwa viwango vya kimataifa vimejitahidi mno kupunguza athari au madhara yatakayo tokana na kemikali zitakazo onekana katika maji


Ukilinganisha na zile za nchi husika . hivyo baada ya kugundua kuwa maji yamekidhi viwango au la hatua ifuatayo ndio itakayohitimisha zoezi zima.



6. KUTOA RIPOTI



Katika hatua hii , ripoti itaandaliwa baada ya kulinganisha majibu tuliyopata na viwango vilivyowekwa mfano ikatokea kwamba kemikali zilizomo kwenye maji ni nyingi ukilinganisha na viwango vilivyowekwa basi fundi husika atatoa mapendekezo kuwa nini kifanyike , mfano kuweka dawa ili kuondoa lilichokuwemo au kutoa katazo kwamba maji yasitumike kabisa yanaweza kusababisho vifo au matatizo ya mda mrefu , baada ya hapo mteja atapewa majibu yake yenye ushauri jinsi gain afanye kutoka na ain ya maji anayotakakutumia .




Ushauri wangu hapa ni kwamba usitumie maji kwa mazoea , hasa matumizi ya kunywa kwa sababu gharama utakazotumia kujitibia zitakuwa kubwa zaidi kuliko pale utakapofuata ushauri wa wataalamu juu ya matumizi


Unaweza kuniandikia au kuomba ushauri juu ya aina ya maji unayotumia , kusudi lako husika , nami nitakushauri


Lengo la blogu hii ni kutoa elimu , juu ya sayansi ya maji na pia kusaidia jamii juu ya matumizi bora na sahihi ya maji ili yaweze kuwa uhai katika maisha yetu ya kila siku na vizazi vijavyo .