Tafuta katika Blogu Hii

Alhamisi, 7 Mei 2015

IJUE KEMIKALI YA CHLORINE



Chlorine ni miongoni mwa elementi za kemikali zinazoaminika sana katika sayansi ya kutibu maji yaani kuua vijidudu hatarishi vya magonjwa katika maji, neno chlorine linatokana na neno la kilatini liitwalo chloros lenye maana rangi ya njano na ukijani kwa mbali hiyo ikiwa ni rangi ya gesi ya chlorine
Ni elementi ya 17 , katika chati ya mpangilio wa elementi , utaijua kwa alama hii (Cl),ikiwa katika kundi liitwalo halojeni,  uzito wa atomu yake ni 35.45g , pia inachemka katika joto la 34.04 nyuzi za sentigredi .
Chlorine inatabia ya kuchukuana na kemikali zingine kwa haraka sana  
Utofauti pekee unaoifanya kemikali hii kuwa bora katika sayansi ya kutibu maji ni kutokana na ukweli kwamba ikiyeyuka katika maji huwa katika mfumo wa kusafiri ikishambulia bacteria waliomo na watakaojitokeza kutokana na maji kukutana na vimelea vya nje vinavyoweza kupenya baada ya mpira wa kusafirishia maji kupasuka , vile vile chlorine hupatikana kilahisi na kwa gharama nafuu ;chlorine inapoyeyuka kwenye maji huwa katika mifumo miwili kitaalamu huitwa hypochlorite na hypochlrous acid hivyo huifanya iendelee kuwepo kwenye maji lakini pia atomu moja ya hydrojeni uondolewa na nitrogen atom uchukua nafasi pale chlorine inapo chukuana na ammonia ambayo ni miongoni mwa gesi zinazokuwepo kwenye maji , hii utokeza chloramines ambazo ni monochloramine , hypochloramine na tetrachloramine , hii uongeza ufanisi wa chlorine kuua vijidudu.








JINSI CHLORINE INAVYOFANYA KAZI
Chlorine inapokuwepo kwenye maji ambapo huwa na  bacteria , huwa  inaenda moja kwa moja kwenye ukuta wa seli wa mdudu na kualibu ukuta huo kisha utawala shughuli zote za hiyo seli ikiua na kutoruhusu mwendelezo wa kizazi wa hiyo seli .
Katika sehemu nyingi ambapo maji hukusanywa kutoka kwenye chanzo chake mfano , mito na hata maziwa ambapo maji hayo husukumwa kwa msukumo Fulani ikitegemea na geografia ya mahali husika hufikishwa sehemu maalumu (treatment plant) , ambapo kunahatua kadhaa maji hupitia kabla ya kuwekwa chlorine , hatua hizo zimeelezwa kwenymakala inayosema  hivi ndivyo maji yenye taka yanavyopitia mfumo wausafishwajikablahayajatumika,
JINSI CHLORINE INAVYOPATIKANA
Kemikali ya chlorine hutengenezwa na makampuni mbali mbali , na upatikana chini ya ardhi ndani ya baadhi ya miamba kemikali hii inaweza kuwa katika hali tofauti tofauti kama vile gesi yabisi na ata kimiminika ,kuna makampuni mengi yanayohusika katika kusambaza na kuuza chlorine ikiwa katika asilimia tofauti,pia ata ubora utofautian hivyo  , na asilimia za malighafi iliyomo mfano utaikutasodium yhpochlorite yenye asilimia 60 kutoka India .
Kiwango cha kemikali hii huwekwa kitaalamu kwenye maji na mafundi sanifu wa maabara ambapo ni lazima kiwango kinachowekwa kiendane na ujazo wa maji yatakayo tibiwa au ikitegemea viwango vya nchi tulivyojiwekea ili isizidi sana au pia isipungue .

MADHARA YA CHLORINE 
Chlorine ina madhara makubwa kwa mwanadamu hasa mtu anapoivuta kama gesi , kihistoria kuna vita iliyopiganwa na watu walitumia chlorine kama silaa , hata juzi tulisikia serikali ya nchi ya syria ikituhumiwa kutumia  gesi ya chlorine dhidi ya waasi , pia siku hadi siku chlorine inamadhara mtu anayefanya kazi pamoja nayo
Chlorine hualibu hasa mapafu , pia mtu anapoimeza kwa kiasi Fulani ukaa ndani ya mwili kwa muda mrefu ikitengeneza athari za kudumu, hivyo ata maji tunayokunywa si kila mtu anaweza kujimiminia tu chlorine kwenye kisima chake kwa kiasi anachotaka bali lazima kuwe na wataalamu wanaofahamu kiasi cha chlorine kinachohitajika , kiwango cha chlorine kisizidi  gramu tano , na chlorine inayosafiri baada ya ile inayohitaji kuwekwa intakiwa isizidi 0.2-0.3 kipimo katika mili lita ,


MAMBO YA KUJUA KUHUSU CHLORINE KABLA YA KUWEKWA KWENYE MAJI

Kitaalamu kemikali hii inapowekwa kwenye maji ni lazima kujua mambo matatu  muhimu ambayo ni
·         Chlorine iliyowekwa
·         Chlorine inayohitajika
·         Chlorine itakayobakia

Jambo hili ni la muhimu sana kwa sababu lazima kuwe na kiwango Fulani cha chlorine kibakie kwenye maji ukiachiliambali kile kilichohitajika na hayo maji , ili kusaidia kuua vijidudu hatarishi kutokana na ukweli kwamba maji yatakayosambazwa hupitia sehemu mbalimbali ambapo kupasuka kwa mipira ya kupielekea maji ni jambo la kawaida hivyo basi itasaidia kumaliza vijidudu vitakavyoingia baada ya mipira hiyo kupasuka

CHLORINE ILIYOWEKWA = CHLORINE INAYOHITAJIKA  + CHLORINE ITAKAYOBAKIA


JINSI YA KUSAFIRISHA CHLORINE

Ktokana na ukweli kwamba chlrine ina react kwa haraka sana hivyo husafirishwa kwa ungalifu wa hali ya juu sana isije ikaleta madhara , hivyo ufungwa kwenye mtungi mikubwa na kwa uhakika  usafiri kwa njia ya treni . ,
Usiache kuacha au kutuma maoni yako , maswali , juu ya maji au kiwanda chako kinavyohitaji au kutumia maji katika uzalishaji kupitia barua pepe yangu ya 

Jumatatu, 27 Aprili 2015

KWA NINI MAJI NI UHAI ?







Mtu akikosa chakula anaweza kuishizaidi ya miezi 2 akinywa maji tu, bali mtuakikosa maji kwa wiki2 tu anaweza kupoteza uhai ,  mwili wa binadamu kwa sehemu kubwa ni maji , Fikilia vile maji maji ambayo yapo mdomoni pale mtu anapokula chakula ikiwa ni hatua ya awali kabisa katika mfumo wa usagaji chakula hali hii uletwa na tezi ambalo huitwa salivary

Pia maji maji yaliyopo katikati ya viungo vya miguu ambayo usaidia mifupa isisagike  pia maji maji hayo usaidia kusinyaa na kutanuka kwa miguu , na ata kuweka msawaziko katika mwendo
Maji pia utokeza sehemu kubwa sana ya damu ambapo oxygen uweza kusafiri ikiwa kwenye mishipa midigo midogo kwa ajili ya shuguri mbali mbali za mwili
Maji hayo katika  uashiria kuwa mwili wa mwanadamu ni  maji kwa kiasi kikubwa 


KAZI ZA MAJI KATIKA MWILI
Mara nyingi nimesikia matabibu na wadau wengi wa sekta ya afya wakisisitiza watu kunywa maji angalau lita tano kwa siku , kutokana na watu wengi hapa duniani tumetingwa na shughuri nyingi hivyo huwa tunajisahau na kujikuta tukinywa kiasi kidogo sana cha maji matokeo yake tumejihisi wagonjwa na hata wengine kukimbilia hospitali kumbe ni kwamba atujazingatia kunywa maji mara kwa mara .

Mada ya hii itazungumzia kazi mbalimbali za maji katika mwili

  1. Maji usaidia kumeng’enya chakula katika mwili
Baada ya kumaliza kula tunahitaji maji , hii ni kwa sababu maji huusika moja kwa moja kusaga chakula , mbali na mmeng’enyo ambao hufanyika maji pia upeleka viini lishe mbalimbali ambavyo huitajika na seli za mwili kuusaidia mwili katika ukuaji au kuboresha zaidi pia maji usaidia kupata choo .

2 . Maji usaidia kuleta msawaziko bora wa kiasi cha joto la mwili
Kwa wastani joto la mwili wa mwanadamu ni 98.6 degree za falenhite au 37 degree za sentigredi , kutokana na shughuli mbali mbali za mwili kiasi cha joto kinaweza kupanda au kushuka , mfano mtu mwenye ugonjwa wa malalia joto lake la mwili linaweza likapanda sana au kupungua , hii kibailogia utokana na seli nyeupe zinazolinda mwili kuzidiwa nguvu na virusi vya ugonjwa hivyo mgonjwa ni lazime anywe maji ya kutosha ili kurekebisha joto la mwili .



3Maji ni muunganiko wa molekuli mbili yaani oxygen na hydrogen ambapo oxygen huitajika na ubongo kwa ajili ya shughuli zake za kila wakati , hivyo basi ili ubongo  uweze kufanya kazi vizuri unahitaji oxygen ambayo utokana na maji tunayokunywa Wakati mwingine tunaweza kuhisi dalili ya kwamba ubongo unahitaji oxygen pale tunapohisi maumivu ya kichwa wengi ukimbilia kutafuta dawa za kutuliza maumivu lakini mimi nashauri watu wajiulize kama walikunywa maji ya kutosha , ingawa si maumivu yote ya kichwa sababu huwa ni kukosa maji .                                                            
4 Maji pia usaidia figo katika kuchuja uchafu na sumu mbali mbali ambapo utolewa nje baada yo uchafu huo kuingia kwenye kibofu cha mkojo  ambapo ni miongoni mwa shughuli za mwili zinazohusisha seli hai .
Unaweza kujua pia kuwa mwili unahitaji  maji pale unapo enda aja ndogo na ukagundua kuwa mkojo umekuwa wemye rangi ya njano naharufu kali

Zote zilizotajwa ni faida za msingi za maji katika kuendeleza uhai wetu hivyo kuna
madhara mengi tutakayo kutana nayo pale tutakapo kosa kunywa maji kwa kiwango kinachotakiwa , mfano kujisikia uchovu , kuumwa kichwa na kukosa choo .
lakini changamoto leo ni je maji yako ni safi na salama ? na kama una uhakika  je utajuaje  ?  ,Ndani ya blogu hii utapata elimu ya kutosha kuhusiana na maji .


Ijumaa, 17 Aprili 2015

JE KWANINI MAJI YA BAHARI YANACHUMVI NYINGI ?



Maji ya bahari hutokana na mkusanyiko wa maji toka vyanzo mbali mbali kama mito , maziwa na ata maji yalioifikia bahari baada ya mvua kunyesha ,




  • Watu wengi wamekuwa wakijiuliza kuwa chumvi nyingi iliyopo katika bahari inatokana na nini hasa?  Mada hii itazungumzia hasa sababu za msingi zinazochangia uwepo wa madini ya chumvi katika bahari napenda kuongelea hili kwa sababu , pindi maji yakitoweka duniani au kupungua je kutakuwa na uwezakano wa kuyatumia ?  zipo nchi ambazo zimefanikiwa kwa kiasi Fulani kupunguza kiasi cha chumvi toka baharini na kuyatumia maji hayo kwa shughuri mbalimbali , pamoja na hayo gharama ya kuyasafisha maji hayo ni kubwa mno ukilinganisha na maji toka vyanzo vingine.

 

Si rahisi kwa maji ambayo yapo juu ya gamba la juu la dunia(fresh water) ambayo yametokana na kunyesha kwa mvua kuingia bahalini na kutokeza chumvi chumvi  kuna njia za msingi tatu ambazo zimeonekan kuwa ni sababishi za uwepo wa chumvi nyingi baharini na miongoni mwa njia hizo zimekuwa za asili hivyo sio rahisi kwa wanasayansi kuzuia visababishi,na hali hii imepelekea pia kiasi cha chumvi ya bahari kiwe kisicho badilika miaka nenda miaka rudi .



Zifuatazo ni njia zinazo ongeza chumvi katika bahari



  1. Kuwepo kwa maozo ya vitu mbalimbali vya asili kama vile wanyama , miti pia shughuri za kibinadamu hasa taka zinazozalishwa uchangia kwa kiasi Fulani , kuna viumbe vya asili vilivyo ozea  ndani ya bahari na vile vilivyoletwa na maji ya mito au maziwa baada ya kuingia baharini  



       2.Baada ya mvua kunyesha au maji yaliyotuama juu ya gamba la dunia hupenya nakuingia ndani ya miamba ambayo huwa na nyufa , nyufa hizo hutokea pale gamba la    ndani la dunia kupata msukumo mzito au mvutano wa asili , maji yanapoingia ndani ya miamba kazi yake kubwa ni kuyeyusha madini yaliyomo ndani ya miamba hiyo miongononi mwa hayo madini huwa ni chloride ambapo huwenda maji yalibeba madini mengine ya sodiam hivyo yanapoungana hutokeza chumvi ya nyumbani (sodiam chloride)

Na hivyo bahari kuwa na chumvi .

Kitu kingine cha kujua ni kwamba ipo mito inayosafiri chini kwa chini nayo huchangia uwepo wa chumvi kama ile mito iliyopo gamba la juu ya uso wa dunia(earth crust)



Yapo pia maziwa ambapo uchangia kuwepo kwa chumvi katika bahari hii ni si ali ya kawaida lakini maziwa hayo ni machache duniani mfano bahari nyekundu , kinachotokea katika maziwa ya kawaida ni kwamba , mito huingia kwanye maziwa nayo yakiwa yamebeba kiasi Fulani cha chumvi ambapo maziwa hayo hupokea maji na kuyatunza kwa muda kisha hutokeza njia ambapo mito hujirudia tena , na hivyo chumvi hupotea kutokana na mzunguko huo , lakini maziwa yenye kiasi kikubwa cha chumvi yenyewe hupokea maji ya mito lakini huwa hayana vinjia vitakavyofanya maji yarudie mito na kuendeleza mzunguko bali maziwa haya hujifanya bahari kwa kusubiri mbaka jua lichemshe maji na mvuke kwenda angani au kupotea hewani , kitendo hicho usababisha chumvi nyingi kubakia katika maziwa hayo .







3        Sababu hii haijatofautiana na ile ya pili isipokuwa hapa huusisha volcano inayotokea baadhi ya sehemu hivyo gamba la chini la dunia huwa kuna joto kali mno ambapohusababisha fukuto la uji wa moto , uji huo ni mkusanyiko wa madini yaliyoyeyusha na maji ya moto ikiwemo chloride ambayo ndio mama wa kutokeza chumvi , hali hii inapotoke huifikia bahari na kuchangia uwepo wa chumvi baharini




Nahitimisha mada hii kwa kusema chumvi ya bahari ni asili yake  kuwepo na kiwango chake akiongezeki wala kupungua ingawa bahari inauwezo wa kijisafisha yenyewe , inawezekana kupunguza chumvi kutoka maji ya bahari pale utakapotaka kuyatumia maji hayo , kama kwenye mapuli ya kuogelea , mada zijazo ntaongelea njia hizo .




Jumatatu, 6 Aprili 2015

HIVI NDIVYO MAJI YENYE TAKA YANAVYOPITIA MFUMO WA USAFISHWAJI KABLA HAYAJATUMIKA



Hapa nitazungumzia maji tunayotumia kila siku kwa matumizi ya nyumbani .
Nchini Tanzania maji tunayotumia hutokana na vyanzo mbali mbali vya maji hasa mito na maziwa , pia kuna mabwawa ya kutengenezwa  mfano bwawa la mindu ambapo pia bwawa hilo hutegemea sana maji kutoka kwenye mito mbali mbali inayotililisha maji kutoka milima ya uruguru . Wizara ya maji ndio imepewa jukumu kubwa hasa la kusimamia na kuendeleza vyanzo hivi kwa umuhimu w taifa letu kiujumla .
Hivyo wizara imegawanya vyanzo hivyo vya maji katika mabonde lakini mada hii haitazungumzia juu ya hayo mabonde .
Maji kutoka kwenye chanzo hubeba vitu mbali mbali ambavyo ndio taka  kama vile mizoga ya wanyama , miti iliyo angushwa na mvua au kwa nji yeyote , vinyesi vya wanyama akiwemo mwanadamu , uchafu kutokana na shughuli mbalimbali za watu kama nyavu za uvuvi , nguo nguo ,  na hata vijidudu viletavyo magonjwa na ata utupwaji wa taka za viwandani .  

ZIFUATAZO NI HATUA ZINAZOFANYIKA ILI KUWEZA KUPATA MAJI YALIYO SAFI NA SALAMA

HATUA ZA AWALI


1 Maji hupita kwenye machujio makubwa au ya kwanza ambapo ukilejea kwenye utangulizi utagundua kuwa maji hubeba taka zenye ukubwa tofauti tofauti hivyo kazi kubwa hasa ya hayo machujio ya kwanza ,
Hivyo baadhi ya taka ndogo ndogo zinaweza kupenya .
Basi watalamu wa maji baada ya kuona hilo wakatengeneza machujio mengine ambapo zile takandogo ndogo zilizo pata nafasi ya kupenya kwenye machujio ya kwanza hapa zimezuiliwa hivyo hubakia chembechembe za taka ambazo  si rahisi kuzichuja kwa hivyo hatua ifuatayo itaonyesha jinsi ya kuondoa hizo chembe chembe za taka



2.Kitaalamu inaeleweka kwamba chembe chembe ndogo za uchafu hubeba chagi hasi hivyo ili tuweze kuziondoa tunahitaji chagi chanya ambapo kitaalamu huitwa coagulant
Kwa hiyo coagulant ni kemikali inayowekwa kwenye maji ili kuungana na chembe ndogo ndogo za uchafu zenye chagi hasi , mfano wa hizo chemikali ni kama Alum au alminuam sulfeti pia ipo nyingine huitwa algae floc ,

3. Hatua hii husisha tanki ambalo linaluhusu maji yetu pamoja na coagulant vipate kuchanganyika na kitendo hicho usababisha chagi hasi na chanya ziungane na kutengeneza mabonge mabonge ya muungano hali hiyo huleta uzito hivyo madonge hayo hushuka chini kabisa ya tanki(basin) ambapo kitaalamu tunasema settlement .
Maji yetu hujitenga mbali na hayo madonge na kuonekana yenye utulivu  kwa juu

HATUA ZA UPILI
 4.Tunanahitaji maji yaweze kujitenga mbali na madonge yaliyo jitenga chini kabisa ya tanki hivyo hatua hii huitwa hatua ya mchujo (filtration) ambapo mji yetu hupelekwa kwenye tanki lingine ambapo kuna vichujio vinavyo husisha leya ya mchanga na leya ya grevos ambapo chembe ndogo za uchafu huchujwa  na madonge ambayo hutolewa na kupelekwa pembeni au dampo maalumu

5. Baada ya hapo maji yetu huonekana yako safi kwa ajili ya kutumia lakini hayapo salama kwa afya zetu kwa sababu bado yatakuwa na vimelea vya magonjwa, kama vile bacteria , virusi amiba nakadhalika , hivyo tunahitaji kuviondoa au kuviua ,hapa ndipo tunahitaji dawa ya kuyatibu maji yetu na kitendo hiki kitaalamu huitwa( disinfection)
Dawa inayoonekana kufanya vizuri zaidi hapa huitwa klorini ambayo inaweza kuwa katika mfumo wa gesi au kimiminika , ingawa mionzi inaweza kutumika kama vile ,
Ultravioleti na Ozoni ,lakini sababu kubwa inayofanya hii kemikali ya klorini iwe bora kuliko zingine ni kwamba inauwezo wa kubaki ikisafiri pindi maji yetu yanapoelekea kwenye jamii ya watumiaji , kwa sababu mipira ya kusambazia maji kuna wakati hupasuka maji yakiwa njiani hivyo  vijidudu hasa bacteria hupata nafasi nyingine ya kudhuru maji yetu hivyo kiasi kidogo sana na kilichopimwa kilicho kati ya mililita 0.2 hadi 0.5 cha dawa hushugulikia hivyo vijidudu .

6. Baada ya hapo maji yetu hupelekwa kwenye tanki kubwa sana ambalo huweza kumudu kubeba maji zaidi ya milioni elfu moja za lita kwa siku kwa ajili ya matumizi ya jamii husika
Hapo ndio mwisho wa jinsi ya kupata maji safi na salama kwa ajiri ya matumizi yetu ya kila siku , ingawa mfumo huu hugharimu kiasi kikubwa sana cha pesa katika kutengenezwa na kufanya ripea hivyo ni muhimu kufanya uangalizi wa mara kwa mara
 Uangalizi huusisha kusafisha machujio baada ya uchujaji kumalizika , kitendo hicho kitaalamu huitwa ( backwashing) tunahitaji kusafisha ili yasije yakaziba na kusababisha hasara na ufanisi usiotakiwa wa mtambo .

Pia uangalizi mwingine ni juu ya kiwango cha dawa ya klorini ambayo inatakiwa ibaki kwenye maji , harufu ya maji , na hata asidiki na ukakasi wa maji



Jumapili, 22 Machi 2015

Maji Kama Rasimali Muhimu Kwako Yanakusaidiaje?

Maji ni rasilimali muhimu na ya pekee sana duniani na mahitaji yake ni makubwa sana , na matumizi yake pia ni makubwa  hivyo basi katika jamii yeyote ile inapotaabika na swala la kukosa maji , maisha huwa ni magumu sana kwa sababu tunahitaji maji katika mambo mengi sana ambapo sitamaliza nikitaja. Dhumuni kuu la blogu hii ni kuelimisha , kutoa ushauri juu ya matumizi bora ya maji na rasilimali zake, Kufanya utafiti juu ya fulsa mbalimbali zinazotokana na maji na pia kufahamu sayansi nzima ya maji katika matumizi mbalimbali  . Katika maisha yetu wanadamu maji huchukua sehemu kubwa sana, wataalamu wa masuala ya mazingira waliwahi kusema kwamba kuna siku ,Dunia itakuwa katika vita vya kugombania maji . Maji hutumika sehemu mbalimbali ikitegemeana na dhumuni la jamii husika , hivyo tunaweza kugawanya katika makundi ya fuatayo .



  1. Matumizi ya nyumbani
  2.  Matumizi ya viwandani
  3.  Matumizi kwa ajili ya umwagiliaji
  4.  Matumizi kwenye mapuli ya kuogelea .



1.MATUMIZI YA NYUMBANI

Nyumbani maaji hutumika kwa ,makusudi mbali mbali lakini muhimu zaidi ni matumizi kwa ajiri ya kunywa , hapa kila binaadamu anahusika matumizi mwngine ya nyumbani ni kama kupikia , kuoshea viombo , kufulia na hata kuogea  hivyo maji kwa matumizi ya nyumbani lazima yawe safi na salama , hasa kwa \ajiri ya kunywa maana ili tuishi lazima tunywe maji , pia tunahitaji maji mazuri ili tusimalize sabuni bila nguo tunazofua kutakata , na hata pale tuchemshapo maji yasiwaze kualibu viombo vya kupikia

Changamoto ni pale hatuwezi kukuta maji tunayoyatumia yako salama kwa matumizi hivyo ni lazima yasafishwe au kutibiwa ?



Njia au mbinu mbalimbali na juhudi za serikali zimekuwa zikifanyika kuhakikisha kwamba watu wanapata maji safi na salama ,

 Kuna matatizo na changamoto mbali mbali ambazo hukwamisha suala hili , na hasa kiuchumi  pale teknologia za kisasa zenye ufanisi mkubwa zinazo tumika nchi zilizoendelea huwa ni ndoto kwa nchi ambazo ndio zina endelea kama Tanzania jambo hil husababisha tujiwekee viwango vyetu wenyewe vya kupunguza madini ambayo hatuyahitaji kwenye maji. Viwango hivyo huwekwa na shirika la viwango nchini huwa si bora ukilinganisha na viwango vya kimataifa ambapo huwekeza pesa ya kutosha na hivyo kukuza teknologia yao .

Pia wakati mwingine siasa huchukua nafasi kubwa hata katika mambo yanayohitaji sayansi

 Wanasayansi wamegundua njia mbalimbali za kusafisha na kuondoa taka na vijidudu hatarishi kwenye maji yaliyo juu ya leya ya juu ya dunia nay ale yaliyo chini ya ardhi



Pia tatizo lingine ni kutothamini wataalamu walio katika sekta hii ya maji hasa watu wa vipimo vya maabara , ambao hufanya kazi katika mazimgira hatarishi hasa kwa afya zao




2            MATUMIZI YA VIWANDANI

..                                                                                                                                  

Matunizi ya viwandani



Maji hutumika viwandani kwa matumizi mbali mbali mfano vipo viwanda vinatumia maji kama malighafi katika utengenezaji wa bidhaa kama vinywaji , vyakula .

Maji pia hutumika viwandani kwa ajili ya kupoozea mitambo , tunajua wazi kwamba baadhi ya mitambo hupata joto kali hivyo maji ni kimiminika kizuli sana kwaajili ya kupooza mitambo hiyo

Tatizo hutokea pale maji ambayo yatatumika bila kuangaliwa ubora wake , hivyo husababisha mdhara makubwa kwenye mitambo hiyo , madhara hayo ni kama kujibandikiza bandikiza kwa madini Fulani kwenye kuta za mitambo , vilevile kubanduka au kukwanguka kwa hizo kuta za hiyo mitambo kwa sababu ya madini Fulani yasiyo hitajika mwisho wa yote hufanisi wake hupungua na kutofanya kazi ipasavyo , mfano kama viwanda vya kutengeneza sukari ambapo huingia gharama kubwa ya kutatua tatizo , au likiwa kubwa zaidi hutakiwa kuagiza mitambo mingine , hivyo kuepuka yote hayo ni lazima tuwe makini kwenye swala la ubora wa maji .

.



              3. MATUMIZI KWA AJILI YA UMWAGILIAJI



Maji yanaweza pia kutumika kwenye kilimo , lakini pia lazima yapimwe kujua kipi hakiitajiki kilichomo kwenye hayo maji ambapo kinaweza kuathiri mmea  hivyo ikasababisha hasara kubwa kwa mtu aliye wekeza kwenye kilimo





               4 .  MATUMIZI KWENYE MAPULI YA KUOGELEA



Maeneo mengi ya starehe na hasa kwenye mahoteli makubwa ambapo utakutana na mabwawa maarumu yaliyojegwa kwa ajili ya kuogelea , usalama na ubora wa hayo maji lazima uzingatiwe ili watumiaji wawe salama mbali na wadudu hatari kwenye maji , na hapa umakini huzingatiwa kwa sababu tu ya kibiashara



  Somo litakalofuata litaelezea  njia za kuondoa na kuua wadudu hatalishi-