Tafuta katika Blogu Hii

Alhamisi, 7 Mei 2015

IJUE KEMIKALI YA CHLORINE



Chlorine ni miongoni mwa elementi za kemikali zinazoaminika sana katika sayansi ya kutibu maji yaani kuua vijidudu hatarishi vya magonjwa katika maji, neno chlorine linatokana na neno la kilatini liitwalo chloros lenye maana rangi ya njano na ukijani kwa mbali hiyo ikiwa ni rangi ya gesi ya chlorine
Ni elementi ya 17 , katika chati ya mpangilio wa elementi , utaijua kwa alama hii (Cl),ikiwa katika kundi liitwalo halojeni,  uzito wa atomu yake ni 35.45g , pia inachemka katika joto la 34.04 nyuzi za sentigredi .
Chlorine inatabia ya kuchukuana na kemikali zingine kwa haraka sana  
Utofauti pekee unaoifanya kemikali hii kuwa bora katika sayansi ya kutibu maji ni kutokana na ukweli kwamba ikiyeyuka katika maji huwa katika mfumo wa kusafiri ikishambulia bacteria waliomo na watakaojitokeza kutokana na maji kukutana na vimelea vya nje vinavyoweza kupenya baada ya mpira wa kusafirishia maji kupasuka , vile vile chlorine hupatikana kilahisi na kwa gharama nafuu ;chlorine inapoyeyuka kwenye maji huwa katika mifumo miwili kitaalamu huitwa hypochlorite na hypochlrous acid hivyo huifanya iendelee kuwepo kwenye maji lakini pia atomu moja ya hydrojeni uondolewa na nitrogen atom uchukua nafasi pale chlorine inapo chukuana na ammonia ambayo ni miongoni mwa gesi zinazokuwepo kwenye maji , hii utokeza chloramines ambazo ni monochloramine , hypochloramine na tetrachloramine , hii uongeza ufanisi wa chlorine kuua vijidudu.








JINSI CHLORINE INAVYOFANYA KAZI
Chlorine inapokuwepo kwenye maji ambapo huwa na  bacteria , huwa  inaenda moja kwa moja kwenye ukuta wa seli wa mdudu na kualibu ukuta huo kisha utawala shughuli zote za hiyo seli ikiua na kutoruhusu mwendelezo wa kizazi wa hiyo seli .
Katika sehemu nyingi ambapo maji hukusanywa kutoka kwenye chanzo chake mfano , mito na hata maziwa ambapo maji hayo husukumwa kwa msukumo Fulani ikitegemea na geografia ya mahali husika hufikishwa sehemu maalumu (treatment plant) , ambapo kunahatua kadhaa maji hupitia kabla ya kuwekwa chlorine , hatua hizo zimeelezwa kwenymakala inayosema  hivi ndivyo maji yenye taka yanavyopitia mfumo wausafishwajikablahayajatumika,
JINSI CHLORINE INAVYOPATIKANA
Kemikali ya chlorine hutengenezwa na makampuni mbali mbali , na upatikana chini ya ardhi ndani ya baadhi ya miamba kemikali hii inaweza kuwa katika hali tofauti tofauti kama vile gesi yabisi na ata kimiminika ,kuna makampuni mengi yanayohusika katika kusambaza na kuuza chlorine ikiwa katika asilimia tofauti,pia ata ubora utofautian hivyo  , na asilimia za malighafi iliyomo mfano utaikutasodium yhpochlorite yenye asilimia 60 kutoka India .
Kiwango cha kemikali hii huwekwa kitaalamu kwenye maji na mafundi sanifu wa maabara ambapo ni lazima kiwango kinachowekwa kiendane na ujazo wa maji yatakayo tibiwa au ikitegemea viwango vya nchi tulivyojiwekea ili isizidi sana au pia isipungue .

MADHARA YA CHLORINE 
Chlorine ina madhara makubwa kwa mwanadamu hasa mtu anapoivuta kama gesi , kihistoria kuna vita iliyopiganwa na watu walitumia chlorine kama silaa , hata juzi tulisikia serikali ya nchi ya syria ikituhumiwa kutumia  gesi ya chlorine dhidi ya waasi , pia siku hadi siku chlorine inamadhara mtu anayefanya kazi pamoja nayo
Chlorine hualibu hasa mapafu , pia mtu anapoimeza kwa kiasi Fulani ukaa ndani ya mwili kwa muda mrefu ikitengeneza athari za kudumu, hivyo ata maji tunayokunywa si kila mtu anaweza kujimiminia tu chlorine kwenye kisima chake kwa kiasi anachotaka bali lazima kuwe na wataalamu wanaofahamu kiasi cha chlorine kinachohitajika , kiwango cha chlorine kisizidi  gramu tano , na chlorine inayosafiri baada ya ile inayohitaji kuwekwa intakiwa isizidi 0.2-0.3 kipimo katika mili lita ,


MAMBO YA KUJUA KUHUSU CHLORINE KABLA YA KUWEKWA KWENYE MAJI

Kitaalamu kemikali hii inapowekwa kwenye maji ni lazima kujua mambo matatu  muhimu ambayo ni
·         Chlorine iliyowekwa
·         Chlorine inayohitajika
·         Chlorine itakayobakia

Jambo hili ni la muhimu sana kwa sababu lazima kuwe na kiwango Fulani cha chlorine kibakie kwenye maji ukiachiliambali kile kilichohitajika na hayo maji , ili kusaidia kuua vijidudu hatarishi kutokana na ukweli kwamba maji yatakayosambazwa hupitia sehemu mbalimbali ambapo kupasuka kwa mipira ya kupielekea maji ni jambo la kawaida hivyo basi itasaidia kumaliza vijidudu vitakavyoingia baada ya mipira hiyo kupasuka

CHLORINE ILIYOWEKWA = CHLORINE INAYOHITAJIKA  + CHLORINE ITAKAYOBAKIA


JINSI YA KUSAFIRISHA CHLORINE

Ktokana na ukweli kwamba chlrine ina react kwa haraka sana hivyo husafirishwa kwa ungalifu wa hali ya juu sana isije ikaleta madhara , hivyo ufungwa kwenye mtungi mikubwa na kwa uhakika  usafiri kwa njia ya treni . ,
Usiache kuacha au kutuma maoni yako , maswali , juu ya maji au kiwanda chako kinavyohitaji au kutumia maji katika uzalishaji kupitia barua pepe yangu ya 

Maoni 8 :

  1. Ukifulia nguo na chroline unaweza kuwa na madhara yoyote?

    JibuFuta
    Majibu
    1. Kwenye nguo inamadhara na sio nguo tu hata kwenye ngozi chafu yenye ukurutu inangarisha.
      Ila nami nahitaji kujua kama kwenye afya ina madhara

      Futa
  2. Nahitaji kujua na madhara yake kwa binadamu

    JibuFuta
  3. Nahitaji kuspray kwa mazingira ya nyumbani kwangu ilikupambana na bacteria wakali waenezao magonjwa nifanyeje

    JibuFuta
  4. Spriti Je,ni Jamii Ya Clorine?

    JibuFuta
  5. Bidhaa inayokuwa imeandikwa Chroline free Ina maana haina Kemikali hii...?

    JibuFuta
  6. Hivi chlorine inaweza kuuwa mchwa wa kwenye kichuguu?

    JibuFuta