- Matumizi ya nyumbani
- Matumizi ya viwandani
- Matumizi kwa ajili ya umwagiliaji
- Matumizi kwenye mapuli ya kuogelea .
1.MATUMIZI YA NYUMBANI
Nyumbani maaji hutumika kwa ,makusudi mbali mbali lakini
muhimu zaidi ni matumizi kwa ajiri ya kunywa , hapa kila binaadamu anahusika
matumizi mwngine ya nyumbani ni kama kupikia , kuoshea viombo , kufulia na hata
kuogea hivyo maji kwa matumizi ya
nyumbani lazima yawe safi na salama , hasa kwa \ajiri ya kunywa maana ili
tuishi lazima tunywe maji , pia tunahitaji maji mazuri ili tusimalize sabuni
bila nguo tunazofua kutakata , na hata pale tuchemshapo maji yasiwaze kualibu
viombo vya kupikia
Changamoto ni pale hatuwezi kukuta maji tunayoyatumia yako salama
kwa matumizi hivyo ni lazima yasafishwe au kutibiwa ?
Njia au mbinu mbalimbali na juhudi za serikali zimekuwa
zikifanyika kuhakikisha kwamba watu wanapata maji safi na salama ,
Kuna matatizo na
changamoto mbali mbali ambazo hukwamisha suala hili , na hasa kiuchumi pale teknologia za kisasa zenye ufanisi
mkubwa zinazo tumika nchi zilizoendelea huwa ni ndoto kwa nchi ambazo ndio zina
endelea kama Tanzania jambo hil husababisha tujiwekee viwango vyetu wenyewe vya
kupunguza madini ambayo hatuyahitaji kwenye maji. Viwango hivyo huwekwa na
shirika la viwango nchini huwa si bora ukilinganisha na viwango vya kimataifa
ambapo huwekeza pesa ya kutosha na hivyo kukuza teknologia yao .
Pia wakati mwingine siasa huchukua nafasi kubwa hata katika
mambo yanayohitaji sayansi
Wanasayansi
wamegundua njia mbalimbali za kusafisha na kuondoa taka na vijidudu hatarishi
kwenye maji yaliyo juu ya leya ya juu ya dunia nay ale yaliyo chini ya ardhi
Pia tatizo lingine ni kutothamini wataalamu walio katika
sekta hii ya maji hasa watu wa vipimo vya maabara , ambao hufanya kazi katika
mazimgira hatarishi hasa kwa afya zao
2 MATUMIZI YA VIWANDANI
..
Matunizi ya viwandani
Maji hutumika viwandani kwa matumizi mbali mbali mfano vipo
viwanda vinatumia maji kama malighafi katika utengenezaji wa bidhaa kama
vinywaji , vyakula .
Maji pia hutumika viwandani kwa ajili ya kupoozea mitambo ,
tunajua wazi kwamba baadhi ya mitambo hupata joto kali hivyo maji ni kimiminika
kizuli sana kwaajili ya kupooza mitambo hiyo
Tatizo hutokea pale maji ambayo yatatumika bila kuangaliwa
ubora wake , hivyo husababisha mdhara makubwa kwenye mitambo hiyo , madhara
hayo ni kama kujibandikiza bandikiza kwa madini Fulani kwenye kuta za mitambo ,
vilevile kubanduka au kukwanguka kwa hizo kuta za hiyo mitambo kwa sababu ya
madini Fulani yasiyo hitajika mwisho wa yote hufanisi wake hupungua na
kutofanya kazi ipasavyo , mfano kama viwanda vya kutengeneza sukari ambapo
huingia gharama kubwa ya kutatua tatizo , au likiwa kubwa zaidi hutakiwa
kuagiza mitambo mingine , hivyo kuepuka yote hayo ni lazima tuwe makini kwenye
swala la ubora wa maji .
.
3. MATUMIZI
KWA AJILI YA UMWAGILIAJI
Maji yanaweza pia kutumika kwenye kilimo , lakini pia
lazima yapimwe kujua kipi hakiitajiki kilichomo kwenye hayo maji ambapo
kinaweza kuathiri mmea hivyo
ikasababisha hasara kubwa kwa mtu aliye wekeza kwenye kilimo
4 . MATUMIZI KWENYE MAPULI YA KUOGELEA
Maeneo mengi ya starehe na hasa
kwenye mahoteli makubwa ambapo utakutana na mabwawa maarumu yaliyojegwa kwa
ajili ya kuogelea , usalama na ubora wa hayo maji lazima uzingatiwe ili
watumiaji wawe salama mbali na wadudu hatari kwenye maji , na hapa umakini
huzingatiwa kwa sababu tu ya kibiashara
Somo litakalofuata
litaelezea njia za kuondoa na kuua
wadudu hatalishi-
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni