MAJI TAKA
Maji taka ni yale maji yaliyogusana na uchafu au kitu
kisichohitajika kwenye maji , yakihusisha mkusanyiko kutoka mahali tofauti tofauti
mfano nyumbani , maji yaliyotumika kuogea ,kufulia , kuoshea viombo na wakati
mwingine yakihusishwa na uwepo wa vinyesi , pia maji haya yanaweza kutoka
viwandani au kwenye taasisi mbalimbali .
Mkusanyiko wote wa maji haya taka hukutana katika bomba moja
kubwa ambalo litasafilisha kuelekea kwenye kumwagwa au kusafishwa na kutibiwa
ili yawe katika kiwango kisicholeta madhara kwenye mazingira
Kumekuwapo na
changamoto juu ya haya maji taka hasa sehemu za
mijini,uwenda hata wewe ukawa mmojawapo kati ya wale waliokutana na kero
ya kuona au hata kukanyaga maji haya machafu wakati ukiwa katika matembezi ,
Maji haya taka ni
hatari hasa pale yanapokutana na mfumo wa maji safi ,ambapo mipira
ya kusambazia maji safi inaweza kupasuka hivyo ikapelekea athari kubwa kwa
watumiaji
SABABU ZA MAJI TAKA KULETA KELO MIJINI
Hapa kuna sababu nyingi zinazosababisha tatizo hili sahemu
za mijini ingawa wapo wanasiasa wanaodai kuwa inatokana na ujenzi unaondelea
kila kukicha katika miji mikubwa hasa ujenzi wa majengo marefu , sitaki kusema
sio kweli lakini kuna ukweli kwa kiasi Fulani kwa sababu niliwahi kushuhudia
binafsi eneo moja muhimu sana la serikali siwezi kulitaja na najua yapo maeneo
mengi kama hayo ambapo mvua iliponyesha nilishangaa kuona maji yakituama eneo
moja na hata kusababisha ofisi niliyokuwa nafanya kazi kuingiliwa na maji ,
nilitafiti ili nijue hasa tatizo liko wapi , ndipo ilionekana wazi kuna chemba
iliyokuwa inapitisha maji taka kuzibwa makusudi ili kuruhusu ujenzi wa majengo
hayo ya serikari . Ilinisikitisha sana kama mtaalamu husika wa maji na
miundombinu yake na hivyo ndivyo ilivyo katika maeneo mengi na sio sababu kubwa
inayoweza kunishawishi kwa sababu ujenzi ukizingatia miundombinu bora ya maji
badala ya kujenga ilimradi tatizo la maji taka mijini litapungua au kwisha
kabisa.
Sababu zifuatazo
zitatuonyesha jibu la msingi na amini usiamini ndivyo ilivyo
1 . Ongezeko la watu sehemu za mijini
Watu wengi wanapojazana sehemu moja wakiwa katika utafutaji
hivyo matumizi ya maji yanakuwa makubwa na maji taka kuwa mengi hii upelekea
miundo mbinu hiyo kuelemewa na kiwango cha taka
au maji yanayosafirishwa
2. Utupaji taka ovyo
Kila mtu anafahamu yakuwa majiji makubwa yana kabiliana na changamoto kubwa ya uchafu kutokana na mamlaka husika kutowajibika ipasavyo katika utatuzi wa tatizo la uchafu hasa jiji letu la Dar es salaam , swala hili pia huendana na tabia mbaya ya mazoea ya baadhi ya watu kutupa taka kama za plastiki ovyo , taka hizi husababisha zile chemba muhimu za kupitisha maji taka kuziba na hivyo maji yanaposhindwa kupita njia iliyopangwa yatatafuta njia mbadala ili yaendelee na safari , hivyo ndivyo watumia barabara na watu wenye shughuri zao mijini wanakutana na kelo ya maji machafu.
3. Uchakavu wa miundo mbinu
Inawezekana kabisa
kuna wakati Fulani miundombinu inayo ruhusu maji taka kupita inatakiwa
kufanyiwa matengenezo au kubadili vifaa vya zamani na kuweka vilivyo kuwa vipya
ilkusaida mfumo endelevu
NINI KIFANYIKE KATIKA KUTATUA TATIZO HILI ?
Njia zifuatazo ni muhimu katia kushughulika na tatizo
1.Kuwe na ujenzi bora utakao zingatia upitishwaji wa maji
safi na maji taka
Hii itasaidia
majitaka kusafiri katika njia zake na hata mafuliko yatakapotokea kusiwe na
athari itakayojitokeza maana mifumo husika itaruhusu maji yasituame . ujenzi
pia utaenda sambamba na ongezeko la watu , hii ni hesabu za takwimu kwamba
miundo mbinu itaweza kubeba maji taka kwa miaka mingi zaidi ikilinganishwa na
ongezeko la watu kila mwaka
2. Mamlaka maalumu pia izingatie swala la usafi ili kuepisha
kuziba kwa chemba za maji taka
Chombo kilichopewa dhamana ya usafi katika majiji makubwa
kihakikishe kina weka vifaa maalumu vya kutunzia taka hasa sehemu za
mikusanyiko ya watu , cha ajabu unaweza ukatembelea vituo vya dara dara hasa
Dar es salaama na usikutane na kitunza uchafu hata kimoja , hii umfanya mtu
aliye na taka mkononi kutupa ovyo , jambo hili pia liende sambamba na elimu juu
ya usafi , hapa kila mmoja anawajibika kumueleza mwenzake juu ya utunzaji wa
mazingira
3. kadri inavyowezekana katika taasisi mbali mbali kuwe na
mifumo ya ndani ya kutibu maji taka badara ya kusafiri umbali mrefu kwa ajili
ya kutibiwa , hii inaweza pia kupunguza gharama na pia inaweza kuzuia kukutana
kwa mfumo wa maji taka na ule wa maji safi .mfano wa mifumo ya ndani ni kama
pondi za maji taka ,
Asante karibu tena kwa mada nyingine nzuri za kukufanya ubadilike juu ya mazingira na hasa matumizi ya maji
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni