Hapa nitazungumzia maji tunayotumia kila siku kwa matumizi
ya nyumbani .
Nchini
Tanzania maji tunayotumia hutokana na vyanzo mbali mbali vya maji hasa mito na
maziwa , pia kuna mabwawa ya kutengenezwa
mfano bwawa la mindu ambapo pia bwawa hilo hutegemea sana maji kutoka
kwenye mito mbali mbali inayotililisha maji kutoka milima ya uruguru . Wizara
ya maji ndio imepewa jukumu kubwa hasa la kusimamia na kuendeleza vyanzo hivi kwa
umuhimu w taifa letu kiujumla .
Hivyo
wizara imegawanya vyanzo hivyo vya maji katika mabonde lakini mada hii
haitazungumzia juu ya hayo mabonde .
Maji kutoka
kwenye chanzo hubeba vitu mbali mbali ambavyo ndio taka kama vile mizoga ya wanyama , miti iliyo angushwa
na mvua au kwa nji yeyote , vinyesi vya wanyama akiwemo mwanadamu , uchafu
kutokana na shughuli mbalimbali za watu kama nyavu za uvuvi , nguo nguo , na hata vijidudu viletavyo magonjwa na ata utupwaji wa taka za viwandani .
ZIFUATAZO
NI HATUA ZINAZOFANYIKA ILI KUWEZA KUPATA MAJI YALIYO SAFI NA SALAMA
HATUA ZA
AWALI
1 Maji hupita kwenye machujio makubwa
au ya kwanza ambapo ukilejea kwenye utangulizi utagundua kuwa maji hubeba taka
zenye ukubwa tofauti tofauti hivyo kazi kubwa hasa ya hayo machujio ya kwanza ,
Hivyo
baadhi ya taka ndogo ndogo zinaweza kupenya .
Basi watalamu wa maji baada ya kuona hilo wakatengeneza machujio mengine ambapo zile
takandogo ndogo zilizo pata nafasi ya kupenya kwenye machujio ya kwanza hapa
zimezuiliwa hivyo hubakia chembechembe za taka ambazo si rahisi kuzichuja kwa hivyo hatua ifuatayo
itaonyesha jinsi ya kuondoa hizo chembe chembe za taka
2.Kitaalamu
inaeleweka kwamba chembe chembe ndogo za uchafu hubeba chagi hasi hivyo ili
tuweze kuziondoa tunahitaji chagi chanya ambapo kitaalamu huitwa coagulant
Kwa hiyo
coagulant ni kemikali inayowekwa kwenye maji ili kuungana na chembe ndogo ndogo
za uchafu zenye chagi hasi , mfano wa hizo chemikali ni kama Alum au alminuam
sulfeti pia ipo nyingine huitwa algae floc ,
3. Hatua
hii husisha tanki ambalo linaluhusu maji yetu pamoja na coagulant vipate
kuchanganyika na kitendo hicho usababisha chagi hasi na chanya ziungane na
kutengeneza mabonge mabonge ya muungano hali hiyo huleta uzito hivyo madonge
hayo hushuka chini kabisa ya tanki(basin) ambapo kitaalamu tunasema settlement
.
Maji yetu
hujitenga mbali na hayo madonge na kuonekana yenye utulivu kwa juu
HATUA ZA
UPILI
4.Tunanahitaji maji yaweze kujitenga mbali na
madonge yaliyo jitenga chini kabisa ya tanki hivyo hatua hii huitwa hatua ya
mchujo (filtration) ambapo mji yetu hupelekwa kwenye tanki lingine ambapo kuna
vichujio vinavyo husisha leya ya mchanga na leya ya grevos ambapo chembe ndogo
za uchafu huchujwa na madonge ambayo
hutolewa na kupelekwa pembeni au dampo maalumu
5. Baada ya
hapo maji yetu huonekana yako safi kwa ajili ya kutumia lakini hayapo salama
kwa afya zetu kwa sababu bado yatakuwa na vimelea vya magonjwa, kama vile
bacteria , virusi amiba nakadhalika , hivyo tunahitaji kuviondoa au kuviua
,hapa ndipo tunahitaji dawa ya kuyatibu maji yetu na kitendo hiki kitaalamu
huitwa( disinfection)
Dawa inayoonekana
kufanya vizuri zaidi hapa huitwa klorini ambayo inaweza kuwa katika mfumo wa
gesi au kimiminika , ingawa mionzi inaweza kutumika kama vile ,
Ultravioleti
na Ozoni ,lakini sababu kubwa inayofanya hii kemikali ya klorini iwe bora
kuliko zingine ni kwamba inauwezo wa kubaki ikisafiri pindi maji yetu
yanapoelekea kwenye jamii ya watumiaji , kwa sababu mipira ya kusambazia maji
kuna wakati hupasuka maji yakiwa njiani hivyo
vijidudu hasa bacteria hupata nafasi nyingine ya kudhuru maji yetu hivyo
kiasi kidogo sana na kilichopimwa kilicho kati ya mililita 0.2 hadi 0.5 cha
dawa hushugulikia hivyo vijidudu .
6. Baada ya
hapo maji yetu hupelekwa kwenye tanki kubwa sana ambalo huweza kumudu kubeba
maji zaidi ya milioni elfu moja za lita kwa siku kwa ajili ya matumizi ya jamii
husika
Hapo ndio
mwisho wa jinsi ya kupata maji safi na salama kwa ajiri ya matumizi yetu ya
kila siku , ingawa mfumo huu hugharimu kiasi kikubwa sana cha pesa katika
kutengenezwa na kufanya ripea hivyo ni muhimu kufanya uangalizi wa mara kwa
mara
Uangalizi huusisha kusafisha machujio baada ya
uchujaji kumalizika , kitendo hicho kitaalamu huitwa ( backwashing) tunahitaji
kusafisha ili yasije yakaziba na kusababisha hasara na ufanisi usiotakiwa wa
mtambo .
Pia
uangalizi mwingine ni juu ya kiwango cha dawa ya klorini ambayo inatakiwa ibaki
kwenye maji , harufu ya maji , na hata asidiki na ukakasi wa maji
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni