TDS ni neno
linalotumika kama msamiati na kifupisho cha maneno ya kiingereza yanayojulikana
kama Total dissolved solids ikimaanisha
kuwa ndani ya maji ambayo yamekutana au kugusana na viwakilishi mbali mbali
kama vya kiumbo , kikemikali au vya kibaiologia
hivyo TDS , huwakilisha mgusano wa maji na chembe chembe za uchafu
zikijumuisha element au kompaundi mbalimbali za kikemikali zilizoweza
kuyeyushwa na maji au zilizotengeneza mgando mgando kutokana maji kushindwa
kuziyeyusha , hivyo basi chembendogo hizo zinakuwa na chaji chanya na hasi pia TDS hujumuisha hata chumvi zisizokuwa za
kioganiki
TDS hutuonyesha picha ya kwamba ni jinsi gani maji yetu
yamechafuka au kukutana na uchafu ingawa ni ngumu kutupa jibu halisi la kiwango
cha uchafuzi hasa katika maji ya
kunywa hivyo mara nyingi tunapokuwatunapima
mahabara TDS hutupa picha ya kwamba
majibu ya vipimo vingine yatakuwaje mfano TDS inapokuwa kubwa tunategemea pia
chloraidi iwepo .
Kiwango kilichowekwa na EPA huko marekanni kuhusu TDS inatakiwa kisizidi milligram 500 katika lita yamaji
JINSI YA KUPIMA TDS KATIKA MAJI
Kwa sababu TDS hujumuisha chembechembe ndogo zilizo na chagi
hasi na chanya hivyo huwa zinatembea zikigongana kwenye maji kila moja ambapo
kitaalamu huita ions kwa jinsi hiyo njia ya kielekroniki hutumika katika kupima
hizo chembe chembe zilizobeba chagi
TDS hupimwa katika miligramu kwa lita moja (mg/l)
Wataalamu wametengeneza kifaa kinachoitwa TDS – Meter ambacho hutumika katika kupimia
Kifaa hicho kimetengenezwa kiasi kwamba huwa na uwezo wa
kuhisi kuwa kuna kiwango gani cha TDS lakini pia kuna mahusiano ya karibu sana
kati ya TDS pamoja na EC neno EC hutokana na neno la kiingereza yaani electric
conductivity ambapo humaanisha uwezo wa maji yenye chembechembe hasi na chanya
kupitisha umeme huwezo huo upimwa katika microsemens per sentimita
Kifaa kwa ajili ya kupima TDS kimetengenezwa kuwa na uwezo
wa kupima na EC pia . ingawa kinaweza kusomwa katika mtindo wa skeli au wa
digitali ikitegemeana na watengenezaji wa kifaa husika walivyotengenezwa , kifaa pia huwa na mahari penye kihisia ambapo kiasi kidogo cha sampuli ya maji
humiminwa ili kujua kiwango cha TDS na EC
Sampuli ya maji inaweza kutibiwa kwanza kabla ya kupima
ikitegemea ni aina gani ya sampuli pia kifaa ni lazima kikaguliwe kama kipo
katika ubora wake
Baada ya kukagua kifaa , kuwa kipo tayali kiasi kidogo cha
sampuli kitamiminwa kwenye kifaa na kubonyeza kitufe cha kupimia ndipo jibu
litaonekana katika mfumo wa digitari au wa skeli ,
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni