Tunaishi kwenye dunia ambayo
kila kitu ni gharama ,hasa yale mahitaji ya msingi ya mwanadamu ikiwemo maji
mahitaji yote haya mwisho wa siku yanatugharimu pesa kutokana na thamani ya tulichotumia
hivyo ni vema kuwa na utaratibu mzuri wa matumizi ili kupunguza gharama
Nitaelezea njia zifuatazo
zitasaidia kabisa kupunguza gharama kama ukizifuata kwa makini
1.kuwa na mita ya kujua kuwa
ni kiasi gani cha maji ulitumia kwa mwezi mzima
Mita za maji ni jambo la
kawaida kwa watu wanaonunua maji kutoka kwa watu binafsi au mamlaka husika za
kiserikali ,lakini kama wewe ni muuzaji wa maji uliye na kisima chako acha kuwa
na biashara ya mazoea nunua mita ili ikusaidie kujua unauza maji ya kiasi gani
kila mwezi , rekodi katika kitabu au mahali popote jumla ya kiwango cha maji
ulichotumia kwa mwezi mzima fanya hivi kila mwezi bila kuacha hii itakupa picha
harisi juu ya maji unayotumia mara kwa mara
2.Orodhesha maji unayotumia
kwa makusudio gani , kuoga ,kufulia nguo , kunywa kusafishia choo au sehemu
mbali mbali za nyumba, umwagiliaji au kuuza , orodha hiyo itakusaidia kufahamu ni maeneo gani ambayo maji yako
yanatumika sana na je kuna unuhimu gani wa hilo eneo maji yakatumika sana , mfano
ukipanga au kuishi kwenye nyumba ambayo hutumia vyoo vinavyohitaji maji mengi
ili kusukuma kinyesi hauna jinsi inaweza kugharimu sana matumizi ya maji hivyo
hakikisha unatumia aina ya choo ambacho hakihitaji maji mengi kama eneo
unaloishi lina tatizo la ukosefu wa maji lakini ukijua kuwa maji yanatumika
sana kuoshea au kufulia unaweza kudhibiti au kupunguza matumizi
3.Hepuka kwenda kwenye bomba
la maji mara kwa mara
Kuna watu kwa sababu tu
wameona kuna bomba linatiririsha maji basi hufungulia kila wakati labda chombo
kimoja au viwili vimechafuka basi mtu ataenda kusafisha huku akiruhusu maji ,
ni vizuri kuweka utaratibu wa kuosha viombo kwa ujumla wake , au badala ya kila
siku kufua nguo moja au mbili ni vizuri kupanga siku maarumu kwa ajili ya kufua
nguo nyingi mbazo utavaa hata zaidi ya wiki moja
4. Kemea na kisha toa elimu
kwa wanafamilia au watumiaji wenza wa maji pale uzembe wa kuruhusu maji yatoke
bila mpango au kwa kujisahau ili watambue utaratibu utakao jiwekea , kila mmoja
anapaswa aelewe juu ya umuhimu wa kutumia maji kwa utaratibu ili kuepusha
gharama za ulipaji
5. Furahia kulipia maji kwa
wakati ili kuepuka usumbufu wa kukatiwa
Unapolipi maji kwa wakati
itakusahidia kufurahia thamani ya ulichokilipia mbali na kulimbikiza unaweza
kujenga hisia baadae kuwa utapaswa kilipia usichostahiri kisha utasema mita
imeenda sana na maji yametumika kidogo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni