Watu wengi ujiuliza
kwamba
PH ya maji ni nini ?
PH ya maji ni neno la
kikemia hutumika kuwakilisha kupimo cha asidiki au ukakasi kilichomo kwenye maji ambapo kiasi hicho cha asidiki au ukakasi upimwa katika mfumo wa ayani
zilizokuwa huru kwenye maji, nazo ni haidrogeni
ayani na zile za haidroksaidi ayani
JINSI YA KUPIMA PH YA MAJI
1.PH ya maji inaweza kupimwa kwa kutumia kifaa maalumu cha
kielekroniki kinachoitwa
PH-mita , kifaa hiki kina umbo dogo kiasi
kwamba fundi sanifu anaweza kwenda nacho kwenye kituo cha kuchukulia sampuli na
akaweza kupima akiwa huko .
TAHADHARI KATIKA MATUMIZI YA KIFAA
Kifaa hiki ili kitoe majibu sahii ni lazima kikaguliwe kabla
ya kutumika , watengenezaji wa kifaa hutoa kumbukumbu muhimu juu ya kifaa
zitakazomsaidia fundi sanifu kukikagu juu ya usahii wake .
Kifaa hutumia kitambuzi ambacho ni elekrodi ili kupima
kiwango cha ayani kwenye sampuli ya maji , hivyo ni muhimu kukikagua na
kukisafisha kila baada ya matumizi lakini mfano wa kitu laini hutumika
kusafishia elektrodi ili iwe katika hali ya kuhisi .
PH- mita
,huifadhiwa kwenye kikasha maalumu kila baada ya kumaliza kukitumia
2. Universal solution . Hii ni chupa kubwa yenye kemikali maalumu inayotumika kupima ph ya
maji ikiwa na lebo inayonyesha rangi tofauti zilizopimwa katika kiwango fulani
cha ph ikianzia 0 mbaka 14, kiwango cha vitone viwili hudondoshwa kwenye kiasi cha mililita kumi
hivi za sampuli ya maji, kisha rangi ubadilika kuendana na sampuli ya maji
ipo kwenye kiasi Fulani cha ph kwa kulinganisha na rangi zilizopo
kwenye lebo ya universal solution .
Pia unaweza kupima PH
kwa kutumia karatasi ndogo zinazopima PH
ya 0 hadi 14 au inayoishia kwenye 12 , vikalatasi hivi huwa kwenye viboxi vidogo
maalumu ambapo uchovywa kwenye
kiasi Fulani cha sampuli na kisha kulinganisha
rangi iliyopangwa kitaalamu na ile ilyotokea .
Kwa nini tunahitaji kujua PH
ya maji ?
Ni muhimu sana kujua pH ya maji kwasababu itatuambia kuwa
nini kimezidi au kimepungua kati ya hali ya uasidi wa maji na hali ya ukakasi
wa maji , mfano kwenye maeneo ambayo
maji ya kunywa yanayowekwa kemikali ya klorini ni muhimu kujua ph ya maji
ambayo kiwango chake huwa kati 6.5—9.0 , kwa sababu maji hayo yanakuwa na
visababishi vyote vya kupanda au kushuka kwa kiwango cha PH
Pia kuna kemikali mbali mbali zinazotumika kuzuia michubuko
au kujibandikiza kwa solidi za kioganiki kwenye viwanda mabapo wana machemshio
au vipoza mitambo ambapo maji yakiwa kwenye ph Fulani kemikali hizo haziwezi kufanya kazi ipasavyo au ili tujue
zimefanya kazi basi PH iwe katika kiwango fulani
Article Mzuri Kwangju congr.vifaa vinapatikana wapi Napa dar?
JibuFutaNi kiwango gani cha ph kinahitajika kwenye maji ya kunywa?
JibuFutaKiwango kizuri ni pH kuanzia 6.9 hadi 7.3 mwishi
JibuFutakwenye mwili wa binadamu ph inaweza kuonekana na kama inaonekana uwa ni ngapi?? kwa kawaida
JibuFuta