Kama ilivyo leo kuna
madaktari wengi ambao wamefungua vituo kwa ajili ya kutoa huduma za afya kwa
jamii lakini si madaktari wote wamekidhi vigezo na masharti kwanza vya wao kuwa
madaktari waliosomea fani hiyo ipasavyo na pili huduma wanayoitoa kwa wateja
wao , kuibuka kwa wimbi la madaktari feki limekuwa tatizo kwenye sekta ya afya
kwani wengi kwanza wamekuwa na gharama kubwa za matibabu kwa wateja na pia
wakati mwingine kutoa maelezo yasiyo ya kweli kwa wagonjwa , pamoja ya kuwa
kuna fulsa ya kujiongezea kipato kwa mtu kuwa na kituo chake cha huduma za afya lakini
taaruma ni vema izingatiwe kuliko kujali pesa , vivyo hivyo ata kwenye suala la ubora
wa maji lina taka ueledi na utaalamu ili kulinda afya za watu , nakumbuka
wakati tuliokuwepo chuoni kimasomo mwalimu wetu aliyetufundisha somo la kutibu maji
alituambia kuwa kama fundi sanifu katika maabara ya maji lazima uwe makini
katika kuzingatia kiwango cha dawa kinachohitajika kwenye maji ili kupambana na
vijidudu , alisema kuwa fundi sanifu anaweza kuua watu wengi kwa mda mfupi
kuliko hata mwanajeshi anayetumia silaha vitani.
Mada hii nimeonelea ni vema
nichapishe kwa sababu kuna mtu alishawahii kuja kuniuliza kuwa yeye maji yake
ni machafu yakiwa na rangi inayoashiria uwepo wa madini ya chuma kwa wingi na
turbidity(chembechembe ndogo za viasili vya kioganiki na vile visivyo vya
kioganiki ) hivyo akaniambia kuwa aliwahi kununua shabu ikiwa kama mawe bila
shaka ni aluminiam sulfate ili kuyasafisha maji hivyo alikuwa na nia ya kuweka
ili asafishe kisima chake alitamani asikie sauti yamgu kama ningemluhusu
aweke, hapa ndipo lile swali ya kwamba
kila mtu anaweza kusafisha maji yake linapopata jibu ya kwamba si kweli hataukipewa kemikaliya klorini uweke kwenye maji
ili kuua vijidudu haitashangaza kusikia umeua watu kwa sababu ya kutokuwa na
utaalamu juu ya maji , hivyo lazime tuheshimu taaruma kuliko kujichukulia hatua
mkononi binafsi naheshimu ninaposikia kuwa mtu katumia miaka kadhaa kusomea
taaruma Fulani mfano nafahamu kuwa nikiumwa kichwa kuna dawa za kutuliza
maumivu lakini unapokutana na daktari aliyetumia muda wake mwingi akiwa shuleni
kusomea magonjwa ya mwanadamu huenda akaniambia tu wala nisitumie dawa ya
kutuliza maumivu bali ninywe maji kwa wingi hivyo kichwa kitapona
HIVI NDIVYO UNAVYOTAKIWA
KUFANYA MAJI YAKO YANAPOKUWA MACHAFU NA UKAHITAJI KUSAFISHA ILI KUUZA AU KWA
MATUMIZI TU YA NYUMBANI
Nilimwambia mteja kuwa usijalibu
kamwe kuweka hiyo dawa kwenye maji bali alitakiwa kuwaona mamlaka husika yaani
wizara ya maji na mamlaka zinazotambulika hivyo lazima wangemwambia ni lazima sampuli ya maji yake
ichukuliwe na kupelekwa maabara iliifanyiwe uchunguzi , pia angeambiwa na
gharama ya kupima maji yake , na endapo taratibu zote zikifuatwa basi majibu
yake yangekuja na ushauri nini kifanyike ili kuyafanya maji yake yawe salama na
safi kwa matumizi
Njia hizo nimewahi kuzieleza
kwenye mada inayosema JINSI YA KUJUA
MAJI NI SAFI NA SALAMA KWA MATUMIZI unaweza kuisoma na ukafahamu jinsi wataalamu watakavyo kusaidia
Endapo kama unahitaji maoni
au ushauri juu ya maji unayotumia unaweza kunitumia barua pepe katika mackthekwembe@gmail.com
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni