FAHAMU KUHUSU MAJI NA SAYANSI YAKE.BLOG SPOT.COM
Lengo la blogi
hii ni kusaidia na kutoa elimu kwa jamii
, hii ni blogi bora ya sayansi Tanzania na Afrika mashariki imeanziswa tarehe
21 /03/2015 ikianza na wasomaji zaidi ya hamsini kwa siku huku ikikua kwa kasi
Blogi hii
imejikita katika utafiti na kutatua changamoto
zinazokumba jamii katika maeneo
mbalimbali ya nchi haswa swala zima la upatikanaji wa maji safi na salama ,kutoa ushauri wa kiteknologia kwa watu wenye
kampuni vikundi na hata mtu mmoja mmoja wanaojihusisha na biashara ambazo
hukutana na changamoto katika swala zima la ubora wa maji au matumizi ya maji
kiujumla mara nyingi swala zima la ubora wa maji limekuwa likimulikwa kwa tochi
au kutopewa kipaumbele hasa nchi zetu zinazoendelea na watu wengi wanapoona maji
yanapatikana kutoka kwenye vyanzo vyao huzania wamemaliza changamoto ,
lakini ukweli unabaki kuwa maji yanaviambatanishi
vingi vinavyoweza kuleta madhara katika afya zetu katika biashara zetu ,viwanda
vyetu na ata katika ujenzi mfano maji
yabisi yanaweza kuleta madhara makubwa kwenye mitambo ya kupozea au ya
kuchemshia ( boilers), kulika kwa chuma . au chumvichumvi kuganda kwenye kuta
za chuma na hivyo kupunguza ufanisi wa mitambo hiyo hii hughalimu makampuni
makubwa kiasi kikubwa cha fedha kutatua tatizo au hulazimika kuagiza mitambo
mingine mfano wa mitambo hiyo ni ile
inayo tumika kwa ajil ya kufua umeme
Pia kiafya maji yenye madini tembo yanaweza
kusababisha kansa kwa mtumiaji kama yataonekana kwa kiwango kidogo tu pia maji
yanaweza kuwa na wadudu hatarishi kiafya , ukuaji wa viwanda na maendeleo ya
kiuchumi huchangia kwa kiasi kikubwa katika uchafuzi pale ambapo madini sumu
yanapotumika kwenye utengenezaji wa vifaa kama kompyuta , vifaa hivi
vinapochakaa , uteketezaji wake unaweza usiwe katika kiwango ambacho ikazuia
yasikutane na vyanzo vya maji
Pia tunatoa
ushauri juu ya kusafisha na kutibu maji ikitegeme dhumuni lako katika matumizi
ya maji hayo
Mfano
Maji kwa matumizi ya kunywa
Maji kwa matumizi ya umwagiliaji
Maji kwa matumizi ya kujengea
Maji kwa matumizi ya viwandani
Maji kwa matumizi ya ufugaji
Pia wasiliana nasi kwa mahitaji
mbali mbali vinavyohusu uchimbaji visima nakadharika
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni