Maji yaonekanavyo inaweza
kuchukuliwa kuwa hakuna shida au madhara yatokanayo lakini , madhara yake ni
makubwa pale madini ya chumvi chumvi yanapo fanikiwa kuingia kwenye mitungi ya machemshio kiasi kwamba
kiwanda kinawaza kufungwa au ikagharimu
pesa nyingi kuhakikisha uzalishaji unaendelea .
Mitungi mikubwa ya kupozea au
kuchemshia hupatwa na athari za maji
magumu pasipo kuangalia ubora wa hayo maji yanayotumika wakati wote hivyo ni jambo
lisilohepukika
MADHARA YATAKAYOJITOKEZA PALE MAJI YENYE UGUMU YATAKAPO TUMIKA KWENYE MACHEMSHIO
Pia maji ambayo hutumika
kutengenezea au kuchanganyia dawa au kemikali kwa ajili ya kuzuia tatizo yanaweza kuchangia tatizo kama hhayaja safishwa vema
Kwa sababu maji yenye ugumu hutokana na chumvi chumvi pale
yanapotumika pasipo uangalifu hivyo ni vizuri kuwekeza kwenye teknologia ya
maabara ya maji itakayosaidia kujua muonekano au ubora wa maji kabla hayajatumika na yafuatayo ni madhara
Ca(HCO3) +
JOTO —› H2O + CO2
(gesi) + CaCO3(Chanzo cha maji magumu au yenye
chumvi chumvi)
kielelezo hapo juu ndio mfano
halisi wa kile kinachotokea kwenye machemshio
kalisiam kaboneti ndio mgando mgando
unaojibandika kwenye kuta za machemshio na hivyo usababisha joto liwe kali sana
kuliko inavyotakiwa lakini pia itakapotoke joto likazidi kupita kiasi
machemshio yatakuwa mbioni kubutuka
Lakini pia majimagumu
yatakapoachwa bila kutibiwa yatasababisha tabia ya kuzua joto lisisambae maeneo yote ya machemshio
Tatizo lisipopatiwa ufumbuzi
inaweza kuzuia ufanisi mzima wa mitungi ya kuchemshia
NJIA ZA KUONDOA MAJI MAGUMU
KABLA HAYAJALETA MADHARA
Kuna njia mbalmbali za kuondoa chumvi chumvi za maji magumu , nji ya kwanza ni kutumi kifaa kinachoitwa
softener ambacho kina uwezo mkubwa wa kuondoa hizo chumvichumvi lakini
kinatumika pale kabla maji hayajaingia kwenye mitungi ya kuchemshia
Mbali na softener tunaweza
pia kutumia RO au reverse osmosis ambapo
kifaa hicho nacho huondoa kiasi kikubwa cha chumvi chumvi na kuzuia athari
kabla ya maji kuingia kwenye mtungi wa kuchemshia
Njia nyingine ni kutumia
chemikali ambazo zina phosphate au kaboneti ndani , polymers kama vile ctalized
silphate
Kama kuna jambo la
kiteknolojia unaweza kuniandikia au kunitumia email ambayo ipo kwenye hii blogi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni