Hivi karibuni kumeibuka kwa ugonjwa wa kipindupindu katika
jiji la Dar es salaam hasa wilaya ya kinondoni ikishika nafasi ya kwanza kwa
kuwa na wagonjwa wengi , ugonjwa huu husababishwa na bacteria anayeitwa
vibrio cholerae , bacteria huyu
hupatikana kwenye kinyesi cha binadamu , hivyo ili upate ugonjwa huu ni lazima
utakuwa umekula kinyesi pasipo kujua pia ugonjwa huu huenezwa na mawakala wa
uchafu hapa nazungumzia mdudu anayeitwa nzi ambaye hupenda kusogelea maeneo
machafu hasa yenye vinyesi vya wanyama , huwenda ulikula tunda ambalo
halikuoshwa ipasavyo au chakula ambacho hakikuhifadhiwa vizuri hivyo nzi
mawakala wakatua kwenye chakula na kuacha vimelea vya magonjwa , lakini kikubwa
zaidi matumizi ya maji ambayo si salama kwa kunywa , niliwai kutembelea baadhi
ya maeneo ya jiji nikiangalia au kukagua ni kipi kisababishi cha ugonjwa huu wa
kipindupindu yapo mengi niliyojifunza lakini kikubwa hasa ni swala zima la
mazingira machafu katika maeneo ya nayozunguka nyumba za watu au sehemu za
kibiashara kama sokoni
SABABU ZIFUATAZO ZILINIFANYA KUANDAA MADA HII KAMA KISABABISHI
1.Miundombinu mibovu ya mfumo wa maji taka na maji safi
Jambo hili nimewahi kuliongelea sana , miundombinu chakavu
ya maji taka usababisha maji taka kukutana na yale yaliyokuwa safi , uwenda ni
yale yaliyotibiwa na dawasco au visima vifupi ambapo watu wamekuwa wakitumia
maji hayo ya visima vifupi wakijua ni chemichemi kumbe ni kuvilia ndani kwa
ndani kwa maji taka lakini hili linaenda sambamba na ukosefu wa vyoo bora
katika baadhi ya maeneo , kuna maeneo ukiingia chooni unaweza ukagairi
kujisaidia hata kama ungebanwa vipi na haja , vyoo chakavu vilivyofikia hatua
ya kutapika ni rafiki kwa nzi wa kijani kubeba vimelea vya magonjwa hasa
kipindupindu
2. uwepe wa maji taka karibu na makazi ya watu
Kuna maeneo mengi sana katikati ya jiji la Dar es salaam
ambapo ni kawaida kukuta maji machafu yakituama kandokando ya makazi ya watu
huku kukiwa na shughuli mbalimbali zikiendelea kama huduma ya vyakura maarufu
kama mama ntilie ,hii pia ni hatari kwa watoto wadogo ambao wakati mwingine
huona maji hayo kama ni sehemu tu ya michezo yao , huenda wasifikie hatua ya
kuyatia kinywani lakini uwezekano wa kugusana nayo mikononi ni mkubwa hivyo wazazi
nao wasipokuwa makini mtoto anaweza kula kitu kingine bila ya kunawa mikono na
kusababisha kupata ugonjwa , sababu hii inaweza kuwa ya msingi kwa sababu
takwimu zimeonyesha kuwa miongoni mwa wagonjwa watoto wamekuwa wengi
ukilinganisha na idadi ya watu wazima
3 .watu kutozingatia kanuni za afya asa usafi binafsi ,
mfano kula chakula bila kunawa vizuri , kunywa maji yasiyotibiwa au kuchemshwa
, pia kama nilivyosema kuhusu watoto ambao awapatiwi uangalizi wa kutosha kutoka
kwa wazazi wanapokuwa katika michezo au katika maswala mazima ya ulaji
4. mkusanyiko mkubwa wa watu katika eneo moja ,
Hapa ndipo chanzo cha ugonjwa , kukua kwa kasi kwani
utagundua nyumba moja ya kupangisha inaweza kuwa na watu wengi au kukaribiana
bila nafasi kati ya nyumba na nyumba hivyo unaweza kuona maeneo hayo maarufu
kama uswailini , wakati mwingine uwezi kutofautisha kuwa choo Fulani ni cha
nyumba hipi , mifumo ya maji taka mara zingine huingiliana kati ya nyumba na
nyumba kiasi kwamba tabia za baadhi ya
watu kutozingatia kanuni za afya upelekea kupatwa na ugonjwa , lakini kwa
sababu watu wamekusanyika eneo moja ni rahisi sana kwao kuambukizana , hivyo ni
vizuri watu wakajaribu kuishi katka maeneo yenyempangilio wa makazi bora
unaoleta maana ya kuishi , mfano mzuri ni wilaya ya ilala ambapo si mara chache
sana hupatwa na kipindupindu ,ingawa pia yapo maeneo hatarishi lakini maeneo
mengi yamepangilika kimakazi
NINI KIFANYIKE KATIKA KUKABILIANA NA UGONJWA HUU HATARI
Katika kutatua au kupambana na tatizo hili kiuna makundi ya
kijamii mashirika binafsi na serikali
1 kijamii
Swala la usafi wa
mazingira linaanza na mtu mmoja mmoja , hasa katika ngazi ya kifamilia , tuache
kuwa wavivu wa kukemea au kusemana kuhusu usafi katika maeneo yetu tunayoishi ,
pia tuache dhana ya kuilaumu serikali bila kufanya sehemu yetu, kama mwanajamii
tunawajibu wa kulinda miundombinu ya maji , wapo watu hukata kwa makusudi
mipira ya kusambazia maji safi ili ajinufaishe wao , si gharama pekee
itakayoingia serikali kufanya matengenezo bali itapelekea kuingiliana kwa
mifumo ya maji safi nay ale ya maji taka
2 serikali au sekta zisizo rasimi nazo zinaweza kuchangia
kuenea kwa ugonjwa kwa namna moja au nyingine , mfano yapo maeneo ambapo hakuna
ufatiliaji juu ya miundombinu chakavu inayopitisha maji safi na maji taka ili
kujua wapi kuna mipasuko inayo sababisha maji yawe na vimelea vya ugonjwa ,
hivyo sampuli za maji zichunguzwe kila baada ya mda Fulani kujua kama kuna
uchafuzi wa maji au la
Pia mamlaka husika kama wizara ya afya inajukumu kubwa la kuhakikisha
elimu ya kutosha inawafikia watu ili wawe na mitazamo mizuri kuelekea afya na
mazingira yao.