Maji ni muhimu sana kwa ajili ya umwagiliaji , katika dunia hii hasa nchi
zinazoendelea, ufanisi na ubora katika swala zima la kilimo ni jambo
linalotazamwa kwa karibu sana , tumefikia wakati ambapo hatuwezi tena kutegemea
mvua ili kufikia kwenye dhima ya uzalishaji bora , hatuwezi tena kutumia jembe
la mkono , pia ardhi yenye rutuba ni jambo la kutazamwa kwa karibu sana , watu
wengi hukumbuka mambo mengi ya msingi wanapofikilia kuanzisha mradi wa kilimo
cha umwagiliaji lakini hawaweki mkazo hasa katika swala zima la ubora wa maji,
wengi wetu huamini tu kuwa kama maji yanapatikana eneo husika basi inatosha
yatumike katika mradi , jambo hilo si sahii kwa sababu maji yanaviwakilishi
vingi ambavyo havihitajiki katika
mmea ili uweze kukua , hivyo lengo la blogi hii ni kukupa ushauri wewe mkulima
uliye na ndoto za kuvuna mazao yaliyo bora pale utakapo fahamu juu ya ubora wa maji yako
, kwani maji yanaweza kuwa na viwakilishi vyenye sumu kali kama vile madini
tembo ,unaweza kuwasiliana nami kupitia barua pepe yangu ambayo ni mackthekwembe@gmail.com kwa maelezo zidi .
Tafuta katika Blogu Hii
Jumapili, 20 Machi 2016
Jumapili, 6 Septemba 2015
KUENEA KWA UGONJWA WA KIPINDUPINDU NA MATUMIZI YA MAJI
Hivi karibuni kumeibuka kwa ugonjwa wa kipindupindu katika
jiji la Dar es salaam hasa wilaya ya kinondoni ikishika nafasi ya kwanza kwa
kuwa na wagonjwa wengi , ugonjwa huu husababishwa na bacteria anayeitwa
vibrio cholerae , bacteria huyu
hupatikana kwenye kinyesi cha binadamu , hivyo ili upate ugonjwa huu ni lazima
utakuwa umekula kinyesi pasipo kujua pia ugonjwa huu huenezwa na mawakala wa
uchafu hapa nazungumzia mdudu anayeitwa nzi ambaye hupenda kusogelea maeneo
machafu hasa yenye vinyesi vya wanyama , huwenda ulikula tunda ambalo
halikuoshwa ipasavyo au chakula ambacho hakikuhifadhiwa vizuri hivyo nzi
mawakala wakatua kwenye chakula na kuacha vimelea vya magonjwa , lakini kikubwa
zaidi matumizi ya maji ambayo si salama kwa kunywa , niliwai kutembelea baadhi
ya maeneo ya jiji nikiangalia au kukagua ni kipi kisababishi cha ugonjwa huu wa
kipindupindu yapo mengi niliyojifunza lakini kikubwa hasa ni swala zima la
mazingira machafu katika maeneo ya nayozunguka nyumba za watu au sehemu za
kibiashara kama sokoni
SABABU ZIFUATAZO ZILINIFANYA KUANDAA MADA HII KAMA KISABABISHI
1.Miundombinu mibovu ya mfumo wa maji taka na maji safi
Jambo hili nimewahi kuliongelea sana , miundombinu chakavu
ya maji taka usababisha maji taka kukutana na yale yaliyokuwa safi , uwenda ni
yale yaliyotibiwa na dawasco au visima vifupi ambapo watu wamekuwa wakitumia
maji hayo ya visima vifupi wakijua ni chemichemi kumbe ni kuvilia ndani kwa
ndani kwa maji taka lakini hili linaenda sambamba na ukosefu wa vyoo bora
katika baadhi ya maeneo , kuna maeneo ukiingia chooni unaweza ukagairi
kujisaidia hata kama ungebanwa vipi na haja , vyoo chakavu vilivyofikia hatua
ya kutapika ni rafiki kwa nzi wa kijani kubeba vimelea vya magonjwa hasa
kipindupindu
2. uwepe wa maji taka karibu na makazi ya watu
Kuna maeneo mengi sana katikati ya jiji la Dar es salaam
ambapo ni kawaida kukuta maji machafu yakituama kandokando ya makazi ya watu
huku kukiwa na shughuli mbalimbali zikiendelea kama huduma ya vyakura maarufu
kama mama ntilie ,hii pia ni hatari kwa watoto wadogo ambao wakati mwingine
huona maji hayo kama ni sehemu tu ya michezo yao , huenda wasifikie hatua ya
kuyatia kinywani lakini uwezekano wa kugusana nayo mikononi ni mkubwa hivyo wazazi
nao wasipokuwa makini mtoto anaweza kula kitu kingine bila ya kunawa mikono na
kusababisha kupata ugonjwa , sababu hii inaweza kuwa ya msingi kwa sababu
takwimu zimeonyesha kuwa miongoni mwa wagonjwa watoto wamekuwa wengi
ukilinganisha na idadi ya watu wazima
3 .watu kutozingatia kanuni za afya asa usafi binafsi ,
mfano kula chakula bila kunawa vizuri , kunywa maji yasiyotibiwa au kuchemshwa
, pia kama nilivyosema kuhusu watoto ambao awapatiwi uangalizi wa kutosha kutoka
kwa wazazi wanapokuwa katika michezo au katika maswala mazima ya ulaji
4. mkusanyiko mkubwa wa watu katika eneo moja ,
Hapa ndipo chanzo cha ugonjwa , kukua kwa kasi kwani
utagundua nyumba moja ya kupangisha inaweza kuwa na watu wengi au kukaribiana
bila nafasi kati ya nyumba na nyumba hivyo unaweza kuona maeneo hayo maarufu
kama uswailini , wakati mwingine uwezi kutofautisha kuwa choo Fulani ni cha
nyumba hipi , mifumo ya maji taka mara zingine huingiliana kati ya nyumba na
nyumba kiasi kwamba tabia za baadhi ya
watu kutozingatia kanuni za afya upelekea kupatwa na ugonjwa , lakini kwa
sababu watu wamekusanyika eneo moja ni rahisi sana kwao kuambukizana , hivyo ni
vizuri watu wakajaribu kuishi katka maeneo yenyempangilio wa makazi bora
unaoleta maana ya kuishi , mfano mzuri ni wilaya ya ilala ambapo si mara chache
sana hupatwa na kipindupindu ,ingawa pia yapo maeneo hatarishi lakini maeneo
mengi yamepangilika kimakazi
NINI KIFANYIKE KATIKA KUKABILIANA NA UGONJWA HUU HATARI
Katika kutatua au kupambana na tatizo hili kiuna makundi ya
kijamii mashirika binafsi na serikali
1 kijamii
Swala la usafi wa
mazingira linaanza na mtu mmoja mmoja , hasa katika ngazi ya kifamilia , tuache
kuwa wavivu wa kukemea au kusemana kuhusu usafi katika maeneo yetu tunayoishi ,
pia tuache dhana ya kuilaumu serikali bila kufanya sehemu yetu, kama mwanajamii
tunawajibu wa kulinda miundombinu ya maji , wapo watu hukata kwa makusudi
mipira ya kusambazia maji safi ili ajinufaishe wao , si gharama pekee
itakayoingia serikali kufanya matengenezo bali itapelekea kuingiliana kwa
mifumo ya maji safi nay ale ya maji taka
2 serikali au sekta zisizo rasimi nazo zinaweza kuchangia
kuenea kwa ugonjwa kwa namna moja au nyingine , mfano yapo maeneo ambapo hakuna
ufatiliaji juu ya miundombinu chakavu inayopitisha maji safi na maji taka ili
kujua wapi kuna mipasuko inayo sababisha maji yawe na vimelea vya ugonjwa ,
hivyo sampuli za maji zichunguzwe kila baada ya mda Fulani kujua kama kuna
uchafuzi wa maji au la
Pia mamlaka husika kama wizara ya afya inajukumu kubwa la kuhakikisha
elimu ya kutosha inawafikia watu ili wawe na mitazamo mizuri kuelekea afya na
mazingira yao.
Jumapili, 16 Agosti 2015
CHANGAMOTO ZA MAJI TAKA KATIKA MAJIJI YANAYOKUWA
MAJI TAKA
Maji taka ni yale maji yaliyogusana na uchafu au kitu
kisichohitajika kwenye maji , yakihusisha mkusanyiko kutoka mahali tofauti tofauti
mfano nyumbani , maji yaliyotumika kuogea ,kufulia , kuoshea viombo na wakati
mwingine yakihusishwa na uwepo wa vinyesi , pia maji haya yanaweza kutoka
viwandani au kwenye taasisi mbalimbali .
Mkusanyiko wote wa maji haya taka hukutana katika bomba moja
kubwa ambalo litasafilisha kuelekea kwenye kumwagwa au kusafishwa na kutibiwa
ili yawe katika kiwango kisicholeta madhara kwenye mazingira
Kumekuwapo na
changamoto juu ya haya maji taka hasa sehemu za
mijini,uwenda hata wewe ukawa mmojawapo kati ya wale waliokutana na kero
ya kuona au hata kukanyaga maji haya machafu wakati ukiwa katika matembezi ,
Maji haya taka ni
hatari hasa pale yanapokutana na mfumo wa maji safi ,ambapo mipira
ya kusambazia maji safi inaweza kupasuka hivyo ikapelekea athari kubwa kwa
watumiaji
SABABU ZA MAJI TAKA KULETA KELO MIJINI
Hapa kuna sababu nyingi zinazosababisha tatizo hili sahemu
za mijini ingawa wapo wanasiasa wanaodai kuwa inatokana na ujenzi unaondelea
kila kukicha katika miji mikubwa hasa ujenzi wa majengo marefu , sitaki kusema
sio kweli lakini kuna ukweli kwa kiasi Fulani kwa sababu niliwahi kushuhudia
binafsi eneo moja muhimu sana la serikali siwezi kulitaja na najua yapo maeneo
mengi kama hayo ambapo mvua iliponyesha nilishangaa kuona maji yakituama eneo
moja na hata kusababisha ofisi niliyokuwa nafanya kazi kuingiliwa na maji ,
nilitafiti ili nijue hasa tatizo liko wapi , ndipo ilionekana wazi kuna chemba
iliyokuwa inapitisha maji taka kuzibwa makusudi ili kuruhusu ujenzi wa majengo
hayo ya serikari . Ilinisikitisha sana kama mtaalamu husika wa maji na
miundombinu yake na hivyo ndivyo ilivyo katika maeneo mengi na sio sababu kubwa
inayoweza kunishawishi kwa sababu ujenzi ukizingatia miundombinu bora ya maji
badala ya kujenga ilimradi tatizo la maji taka mijini litapungua au kwisha
kabisa.
Sababu zifuatazo
zitatuonyesha jibu la msingi na amini usiamini ndivyo ilivyo
1 . Ongezeko la watu sehemu za mijini
Watu wengi wanapojazana sehemu moja wakiwa katika utafutaji
hivyo matumizi ya maji yanakuwa makubwa na maji taka kuwa mengi hii upelekea
miundo mbinu hiyo kuelemewa na kiwango cha taka
au maji yanayosafirishwa
2. Utupaji taka ovyo
Kila mtu anafahamu yakuwa majiji makubwa yana kabiliana na changamoto kubwa ya uchafu kutokana na mamlaka husika kutowajibika ipasavyo katika utatuzi wa tatizo la uchafu hasa jiji letu la Dar es salaam , swala hili pia huendana na tabia mbaya ya mazoea ya baadhi ya watu kutupa taka kama za plastiki ovyo , taka hizi husababisha zile chemba muhimu za kupitisha maji taka kuziba na hivyo maji yanaposhindwa kupita njia iliyopangwa yatatafuta njia mbadala ili yaendelee na safari , hivyo ndivyo watumia barabara na watu wenye shughuri zao mijini wanakutana na kelo ya maji machafu.
3. Uchakavu wa miundo mbinu
Inawezekana kabisa
kuna wakati Fulani miundombinu inayo ruhusu maji taka kupita inatakiwa
kufanyiwa matengenezo au kubadili vifaa vya zamani na kuweka vilivyo kuwa vipya
ilkusaida mfumo endelevu
NINI KIFANYIKE KATIKA KUTATUA TATIZO HILI ?
Njia zifuatazo ni muhimu katia kushughulika na tatizo
1.Kuwe na ujenzi bora utakao zingatia upitishwaji wa maji
safi na maji taka
Hii itasaidia
majitaka kusafiri katika njia zake na hata mafuliko yatakapotokea kusiwe na
athari itakayojitokeza maana mifumo husika itaruhusu maji yasituame . ujenzi
pia utaenda sambamba na ongezeko la watu , hii ni hesabu za takwimu kwamba
miundo mbinu itaweza kubeba maji taka kwa miaka mingi zaidi ikilinganishwa na
ongezeko la watu kila mwaka
2. Mamlaka maalumu pia izingatie swala la usafi ili kuepisha
kuziba kwa chemba za maji taka
Chombo kilichopewa dhamana ya usafi katika majiji makubwa
kihakikishe kina weka vifaa maalumu vya kutunzia taka hasa sehemu za
mikusanyiko ya watu , cha ajabu unaweza ukatembelea vituo vya dara dara hasa
Dar es salaama na usikutane na kitunza uchafu hata kimoja , hii umfanya mtu
aliye na taka mkononi kutupa ovyo , jambo hili pia liende sambamba na elimu juu
ya usafi , hapa kila mmoja anawajibika kumueleza mwenzake juu ya utunzaji wa
mazingira
3. kadri inavyowezekana katika taasisi mbali mbali kuwe na
mifumo ya ndani ya kutibu maji taka badara ya kusafiri umbali mrefu kwa ajili
ya kutibiwa , hii inaweza pia kupunguza gharama na pia inaweza kuzuia kukutana
kwa mfumo wa maji taka na ule wa maji safi .mfano wa mifumo ya ndani ni kama
pondi za maji taka ,
Asante karibu tena kwa mada nyingine nzuri za kukufanya ubadilike juu ya mazingira na hasa matumizi ya maji
Jumapili, 9 Agosti 2015
FAHAMU KUHUSU ALGAE FLOC
Ni dawa inayotumika katika
sayansi ya kutibu maji , iliyotengenezwa kutokana na vijidudu vinavyoitwa algae
,algae ni miongoni mwa viumbe hai vyenye ukijani kama majani
Wakati maji yamepitia njia
tofauti tofauti ya usafishwaji .Kazi moja kubwa ya algae floc ni kusafisha
maji ambayo yamejumuisha taka ndogo sana ambazo zilifanikiwa kupenya kupitia
kwenye machujio , taka zote zenye umbo dogo hukusanywa na algaefloc mbayo
hutokeza mabonge ambayo mwisho huzama chini kwa nguvu ya mvutano tayari
kuondolewa nje ya tanki kwenda kutupwa kama uchafu
Jumapili, 2 Agosti 2015
FAHAMU NJIA BORA ZA MATUMIZI YA MAJI ILI KUPUNGUZA GHARAMA YA KULIPIA
Tunaishi kwenye dunia ambayo
kila kitu ni gharama ,hasa yale mahitaji ya msingi ya mwanadamu ikiwemo maji
mahitaji yote haya mwisho wa siku yanatugharimu pesa kutokana na thamani ya tulichotumia
hivyo ni vema kuwa na utaratibu mzuri wa matumizi ili kupunguza gharama
Nitaelezea njia zifuatazo
zitasaidia kabisa kupunguza gharama kama ukizifuata kwa makini

1.kuwa na mita ya kujua kuwa
ni kiasi gani cha maji ulitumia kwa mwezi mzima
Mita za maji ni jambo la
kawaida kwa watu wanaonunua maji kutoka kwa watu binafsi au mamlaka husika za
kiserikali ,lakini kama wewe ni muuzaji wa maji uliye na kisima chako acha kuwa
na biashara ya mazoea nunua mita ili ikusaidie kujua unauza maji ya kiasi gani
kila mwezi , rekodi katika kitabu au mahali popote jumla ya kiwango cha maji
ulichotumia kwa mwezi mzima fanya hivi kila mwezi bila kuacha hii itakupa picha
harisi juu ya maji unayotumia mara kwa mara
2.Orodhesha maji unayotumia
kwa makusudio gani , kuoga ,kufulia nguo , kunywa kusafishia choo au sehemu
mbali mbali za nyumba, umwagiliaji au kuuza , orodha hiyo itakusaidia kufahamu ni maeneo gani ambayo maji yako
yanatumika sana na je kuna unuhimu gani wa hilo eneo maji yakatumika sana , mfano
ukipanga au kuishi kwenye nyumba ambayo hutumia vyoo vinavyohitaji maji mengi
ili kusukuma kinyesi hauna jinsi inaweza kugharimu sana matumizi ya maji hivyo
hakikisha unatumia aina ya choo ambacho hakihitaji maji mengi kama eneo
unaloishi lina tatizo la ukosefu wa maji lakini ukijua kuwa maji yanatumika
sana kuoshea au kufulia unaweza kudhibiti au kupunguza matumizi
3.Hepuka kwenda kwenye bomba
la maji mara kwa mara
Kuna watu kwa sababu tu
wameona kuna bomba linatiririsha maji basi hufungulia kila wakati labda chombo
kimoja au viwili vimechafuka basi mtu ataenda kusafisha huku akiruhusu maji ,
ni vizuri kuweka utaratibu wa kuosha viombo kwa ujumla wake , au badala ya kila
siku kufua nguo moja au mbili ni vizuri kupanga siku maarumu kwa ajili ya kufua
nguo nyingi mbazo utavaa hata zaidi ya wiki moja
4. Kemea na kisha toa elimu
kwa wanafamilia au watumiaji wenza wa maji pale uzembe wa kuruhusu maji yatoke
bila mpango au kwa kujisahau ili watambue utaratibu utakao jiwekea , kila mmoja
anapaswa aelewe juu ya umuhimu wa kutumia maji kwa utaratibu ili kuepusha
gharama za ulipaji
5. Furahia kulipia maji kwa
wakati ili kuepuka usumbufu wa kukatiwa
Unapolipi maji kwa wakati
itakusahidia kufurahia thamani ya ulichokilipia mbali na kulimbikiza unaweza
kujenga hisia baadae kuwa utapaswa kilipia usichostahiri kisha utasema mita
imeenda sana na maji yametumika kidogo
Jumapili, 26 Julai 2015
REVERSE OSMOSIS
RO huondoa chembe ndogo ndogo za uchafu pale maji
yanayosafishwa hupita katika kiwambo chembamba ambachokinaweza kuruhusu maji
yakiwa pekeyake bila uchafu
Kinachotoke ni kwamba maji ambayo yana kiwango Fulani cha
chumvi au madini mengine husukumwa na
msukumo mkali kupita kwenye kiwambo chembamba hivyo msukumo hupungua pale
yanapo toka yakiwa katika hali bora
Vifaa vya RO huwa na uwezo wa kufanya kazi katika
msukumo wa kati ya 200 - 800
psig
Pia RO imetengenezwa kiasi kwamba maji yanatibiwa dhidi ya
bacteria kwa kutumia mionzi ya uv ingawa
pia kiwambo chembamba kinachoruhusu maji yasiyo na chumvi iliyoyeyuka kupenya
ina vitundu ambavyo vinaweza kutoruhusu bacteria kupenya hivyo wakaondolewa kwa
njia ya kawaida
JINSI RO INAVYOFANYA KAZI
Mada iliyopita nilielezea maana ya RO hivyo hapa nitaelezea
jinsi gani mtambo huu ufanya kazi , lengo langu ni kwamba msomaji wa blogu hii
upate kuelewa kwa namna Fulani juu ya RO
Maji kutoka kwenye chanzo huingia kwenye maifazio na kisha
kuruhusiwa kwenda kwenye mtambo ili kazi ya kusafishwa iweze kuanza kitendo cha asili yaani osmosis huitaji maji
yaliyo katika msukumo mdogo kwenda kwenye yale yaliyo na msukumo mkubwa
yakipita kwenye kiwambo chembamba cha matilio maalumu ya kuchuja
Neno reverse humanisha kinyume hivyo kifaa hiki uruhusu maji yenye mgandamizo mkubwa kwenda
mdogo kwa msaada wa pampu ambayo usaidia katika msukumo na hivyo ndivyo maji
yanapochujwa hivyo maji yenye mgandamizo mkubwa huelekea kwenye eneo lenye mgandamizo
mdogo hivyo msukumo mkubwa ndio utakao
sababisha chumvi iliyoyeyuka iweze kuondolewa kwa kiwango kikubwa , wataalamu
huamini kuwa RO inaweza kuondoa asilimia 95 hadi 99 za chumvi iliyoyeyuka
Pia ufanisi unapoonekana umepungua tatizo linaweza kuwa viwambo
vyembamba vikawa vimezidiwa uwezo wa kuchuja au kuondoa chumvi iliyoyeyuka
hivyo huitajika vibadilishwe
Jumapili, 12 Julai 2015
REVERSE OSMOSIS
RO ni kifaa cha kisasa kinachotumika kuondoa chumvichumvi
ambayo hutokeza maji magumu , mada
zilizopita nilielezea madhara ya maji magumu
Kifaa hiki kimetengenezwa kiasi kwambwa kina uwezo wa kuvuta
chuvi chumvi yote na kuyaacha maji yakiwa salama
Lakini uwezo wa
kuondoa chumvi hutofautiana kwa kifaa kimoja na kingine ikitegemeana na kiwango
cha chumvi
Pia RO imetengenezwa kiasi kwamba maji yanatibiwa dhidi ya
bacteria kwa kutumia mionzi ya uv
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)



