RO huondoa chembe ndogo ndogo za uchafu pale maji
yanayosafishwa hupita katika kiwambo chembamba ambachokinaweza kuruhusu maji
yakiwa pekeyake bila uchafu
Kinachotoke ni kwamba maji ambayo yana kiwango Fulani cha
chumvi au madini mengine husukumwa na
msukumo mkali kupita kwenye kiwambo chembamba hivyo msukumo hupungua pale
yanapo toka yakiwa katika hali bora
Vifaa vya RO huwa na uwezo wa kufanya kazi katika
msukumo wa kati ya 200 - 800
psig
Pia RO imetengenezwa kiasi kwamba maji yanatibiwa dhidi ya
bacteria kwa kutumia mionzi ya uv ingawa
pia kiwambo chembamba kinachoruhusu maji yasiyo na chumvi iliyoyeyuka kupenya
ina vitundu ambavyo vinaweza kutoruhusu bacteria kupenya hivyo wakaondolewa kwa
njia ya kawaida
JINSI RO INAVYOFANYA KAZI
Mada iliyopita nilielezea maana ya RO hivyo hapa nitaelezea
jinsi gani mtambo huu ufanya kazi , lengo langu ni kwamba msomaji wa blogu hii
upate kuelewa kwa namna Fulani juu ya RO
Maji kutoka kwenye chanzo huingia kwenye maifazio na kisha
kuruhusiwa kwenda kwenye mtambo ili kazi ya kusafishwa iweze kuanza kitendo cha asili yaani osmosis huitaji maji
yaliyo katika msukumo mdogo kwenda kwenye yale yaliyo na msukumo mkubwa
yakipita kwenye kiwambo chembamba cha matilio maalumu ya kuchuja
Neno reverse humanisha kinyume hivyo kifaa hiki uruhusu maji yenye mgandamizo mkubwa kwenda
mdogo kwa msaada wa pampu ambayo usaidia katika msukumo na hivyo ndivyo maji
yanapochujwa hivyo maji yenye mgandamizo mkubwa huelekea kwenye eneo lenye mgandamizo
mdogo hivyo msukumo mkubwa ndio utakao
sababisha chumvi iliyoyeyuka iweze kuondolewa kwa kiwango kikubwa , wataalamu
huamini kuwa RO inaweza kuondoa asilimia 95 hadi 99 za chumvi iliyoyeyuka
Pia ufanisi unapoonekana umepungua tatizo linaweza kuwa viwambo
vyembamba vikawa vimezidiwa uwezo wa kuchuja au kuondoa chumvi iliyoyeyuka
hivyo huitajika vibadilishwe