Unapotaka kujua kuwa maji
yako yanafaa au hayafai kwa matumizi lazime kuzingatia kuwa ni nini kusudi la
kutumia maji yako .Je ni kwa ajiri ya kunywa na matumizi ya nyumbani , kwa
ajiri ya ujenzi , au kwa ajiri ya mapuli ya kuogela ?
Maji kabla hayajatua katika
gamba la juu la dunia yakiwa kama mvua yanakuwa katika usalama ila pale
yanapoifikia tu ardhi ndipo uhakika wa usalama wake ni sifuri , hii ni kwa
sababu kuna mgusano wa mambo mengi ambayo yapo ardhini na maji yanapoifikia ardhi , mfano kuna
madini mbali mbali kama vile aluminiam ,calcium na chembechembe za kioganiki ,
bila kusahau bacteria mbalimbali , ambao ukaa kwenye vinyesi vya wanyama damu
moto mfano vibrio cholera . lakini ni mara ngapi tumewahi kuhisi au kuamini
kuwa maji ya chanzo Fulani kama chemichemi ni safi na salama na wakati mwingine
tumejalibu kunywa bila hata kuchemsha ? hasa sehemu za vijijini watu wengi
wamekuwa wakiishi kwa mazoea , hii imefanya ata kinga zao kukubaliana na
mazingira ya maji wanayo yatumia , bila kuhisi kuumwa kwa muda mrefu , lakini
angalizo ni kwamba , watu hao wapo kwenye hatari ya kuugua magonjwa
yanayotokana na maji kama vile kipindupindu
Je tutajuaje sasa kuwa maji
tunayoyatumia ni safi na salama ?
Hapa nitaelezea hatua za
awali mbaka ile ya mwisho ambayo itatupatia hitimisho
1 KUFAHAMU CHANZO CHA MAJI HUSIKA
Chanzo
gani ambacho kina maji yanayotumiwa , chanzo kinaweza kuwa mto , ziwa au bwawa
la kutengenezwa , kisima ,bomba la maji yakusambazwa au maji ya bahari , lengo
la kujua chanzo kinaweza kutupa historia ya eneo husika , lakini kikuubwa zaidi
ni ili tupate kuchukua sampuli ambayo itawakilisha chanzo kizima , pia tujue ni
vifaa gani vya kwenda navyo kwenye kituo husika ili tuchukue sampuli ,neno sampuli humaanisha kiasi kidogo
cha kitu unakichukua kwaajiri ya kufanyia utafiti fulani lakini pindi utakapo pata jibu la kile unachokitafuta basi hiyo sampuli itawakilisha kitu kikubwa , mfano sampuli ya damu ya mnyama inaweza kuwa kiasi kidogo lakini ikawakilisha damu yote ya mwilini labda ikatolewa kwa ajili ya utafiti wa magonjwa, vivyo hivyo ni sawa na maji pia .
2
UCHUKUAJI WA
SAMPULI ZA MAJI
Katika kuchukua sampuli ya maji kunatofautiana
kutokana na aina ya chanzo cha maji mfano
jinsi utakavyochukua sampuli ya maji ya mtoni ni tofauti na vile
utakavyochukua sampuli ya kisima , pia hata ile ya bombani ,pia kuna chupa
maalumu za kubebea sampuli nazo chupa hutofautiana ikitegemea nini
kitakachoangaliwa kwenye maji ya chanzo husika mfano utakapo chukua sampili ya
maji ili kujua kiwango gani cha hewa ya oxigeni kilichotumiwa na bacteri ili
kuvunja vunja vitu vilivyooza ni lazima chupa yake iwe isiyopitisha mwanga wa
jua ili kuzuia bacteria wasifanye kazi ndani ya maji hapa sitaelezea jinsi ya
kuchukua sampuli ya vyanzo mbali mbali bali itakuwa ni mada itakayojitegemea
wakati mwingine , lakini mkazo hapa , ili kupata majibu yaliyo sahii ni vema
kuzingatia njia za uchukuaji wa sampuli na si kila mtu anaweza kuchukua sampuli bali ni
mafundi sanifu wa maabara au mtu aliyepata mafunzo maalumu , baada ya kuchukua
sampuli husika ni vema kukumbuka kufunga vifuniko vya chupa vizuri ili
kutoruhusu kitu tofauti cha nje kuingia na pia kwa usalama wa sampuli isije
kumwagika wakati wa safari ya kurudi
3
KUBANDIKA LEBO
KATIKA KILA SAMPULI
Ni kitu muhimu sana kubandika lebo katika kila
chupa ya sampuli iliyokusanywa , hapa lebo itaonyesha ni muda gani sampuli ilichukuliwa
na tarehe , chanzo cha sampuli mto bomba au kisima , jina la mtu aliyechukua
sampuli , na mwisho kama sampuli inahitaji kutunzwa kwenye mazingira fulani ili
isije kupoteza uhalisia wake
4.
SAMPULI KUFIKISHWA MAABARA ILI ICHUNGUZWE
Hapa kabla sampuli ya maji
haijachunguzwa lazima isajiliwe , kuwa
inatoka wapi , ni aina gani ya chanzo cha sampuli , pia nini kinachotakiwa
kichunguzwe kwenye hiyo sampuli
Hapa sampuli ukutana na watu
wengine tofauti walioajiriwa kwa kazi hiyo ya kusajiri sampuli na uwenda
ikapewa namba ya utambulisho ili majibu yatakapo patikana yapelekwe mahali
sampuli ilipotoka ili kuzuia kuchanganywa
Baada ya kusajiliwa kwa
sampuli ,ni lazima maabara iwe tayali kwa ajili ya kufanya uchunguzi , hapa
lazima wawepo mafundi sanifu ambao watabaki pindi wengine walipoenda kuchukua
sampuli ili kuweka maabara katika hari safi na ya usalama ili kufanya kazi ,
mfano vifaa , vitakavyotumika viwe kwenye usafi na visivyo na matatizo , pia
chemikali ziwe zimestandadaiziwa vizuri , sampuli upimwa kwa umakini ilikujua
nini kilichomo au kinachokusudiwa , zipo njia mbili kuu zitakazotupa majibu ya
kile tunachokitafuta katika maabara , yaani
·
Kutumia vifaa
vinavyotoa majibu kidigitari
·
Na ile
inayohusisha titresheni ambapo kemikali huusika sana
Ingawa kwa uchunguzi wa
kibailogia huwa tofauti na njia hizo kuu mbili , kwa sababu husisha kuotesha wadudu hivyo majibu upatikana kwa kila sampuli ingawa majibu mengine
yanaweza kuchukua siku zaidi ya moja kwa kuwa wadudu
wanaoteshwa kwa kupewa chakura Fulani , na katika jotolidi Fulani
5. ULINGANIFU WA MAJIBU NA
VIWANGO VYA NCHI HUSIKA AU VYA KIMATAIFA
Baada ya maji kupimwa
kitaalamu na kwa umakini mkubwa majibu yatakayopatikana ni lazima yalinganishwe
na viwango vya nchi husika au vya WHO yaani kimataifa hii ni kutoka na ukweli
kwamba si kila nchi inaweza kufiti viwango vya kimataifa kutokana na hali ya
uchumi , ingawa utagundua kuwa viwango vya kimataifa vimejitahidi mno kupunguza
athari au madhara yatakayo tokana na kemikali zitakazo onekana katika maji
Ukilinganisha na zile za nchi
husika . hivyo baada ya kugundua kuwa maji yamekidhi viwango au la hatua
ifuatayo ndio itakayohitimisha zoezi zima.
6. KUTOA RIPOTI
Katika hatua hii , ripoti
itaandaliwa baada ya kulinganisha majibu tuliyopata na viwango vilivyowekwa
mfano ikatokea kwamba kemikali zilizomo kwenye maji ni nyingi ukilinganisha na
viwango vilivyowekwa basi fundi husika atatoa mapendekezo kuwa nini kifanyike ,
mfano kuweka dawa ili kuondoa lilichokuwemo au kutoa katazo kwamba maji
yasitumike kabisa yanaweza kusababisho vifo au matatizo ya mda mrefu , baada ya
hapo mteja atapewa majibu yake yenye ushauri jinsi gain afanye kutoka na ain ya
maji anayotakakutumia .
Ushauri wangu hapa ni kwamba
usitumie maji kwa mazoea , hasa matumizi ya kunywa kwa sababu gharama
utakazotumia kujitibia zitakuwa kubwa zaidi kuliko pale utakapofuata ushauri wa
wataalamu juu ya matumizi
Unaweza kuniandikia au kuomba
ushauri juu ya aina ya maji unayotumia , kusudi lako husika , nami nitakushauri
Lengo la blogu hii ni kutoa
elimu , juu ya sayansi ya maji na pia kusaidia jamii juu ya matumizi bora na
sahihi ya maji ili yaweze kuwa uhai katika maisha yetu ya kila siku na vizazi
vijavyo .